Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Rais wa Catalonia afuta nia yake ya kuitisha uchaguzi wa haraka

Rais wa Catalonia Carles Puigdemont ambaye siku ya Alhamisi alitarajiwa kuhutubia wananchi wa eneo hilo kuhusu kuitisha uchaguzi wa haraka wa uhuru wa jimbo hilo ameamua kuachana na uwezekano huo.

Rais wa Catalonia Carles Puidgemont ameamua kujizuia kuitisha uchaguzi wa katika eneo hilo uliotarajiwa kufanyika manmo mwezi Desemba, wakati wa hotuba yake, Barcelona, Oktoba 26, 2017.
Rais wa Catalonia Carles Puidgemont ameamua kujizuia kuitisha uchaguzi wa katika eneo hilo uliotarajiwa kufanyika manmo mwezi Desemba, wakati wa hotuba yake, Barcelona, Oktoba 26, 2017. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa jimbo la Catalonia nchini Uhispania, ulitarajiwa kutisha Uchaguzi mpya wa wabunge wa jimbo hilo.

Ripoti zinasema kuwa, Uchauzi huo ulikua unatarajiwa kufanyika tarehe 20 mwezi Desemba, na ungelilenga kuhakikisha kuwa jimbo hilo linajitenga kabisa na Uhispania.

Aidha, uongozi huo unatarajiwa kutoa tangazo la eneo hilo kujitenga, hatua ambazo zinapingwa vikali na serikali ya Madrid.

Mapema wiki hii Uhispania ilitangaza kwamba itachukua hatua za kufutilia mbali utawala wa Catalonia ikiwa kiongozi wake hataachana na hatua za kutafua uhuru, naibu waziri mkuu amesema.

Soraya Sáenz de Santamaría alitoa onyo siku moja moja kabla ya siku aliyopewa Carles Puigdemont, kumalizika.

Serikali ya Catalonia imesisitiza kuwa haiwezi kutekeleza matakwa ya Madrid baada ya kura iliyokumbwa na utata ya Catalonia.

Kumekuwa na maandamano kupinga kuzuiwa kwa viongozi wa vugugu la Catalonia.

Jordi Sánchez na Jordi Cuixart wanazuiliwa huku wakichunguzwa kwa uhaini - hatua ambayo upande ambao unataka uhuru unaiona kuwa iliochochewa kisiasa.

Hivi karibuni mrengo unaotaka kujitenga eneo la Catalonia, ulitangaza kuwa ikiwa serikali kuu ya nchi hiyo itamuuzulu kiongozi wao, basi utaanzisha uasi wa kiraia.

Muungano huo unaoyajumuisha mashirika ya zimamoto, walimu na wanafunzi wa vyuo vikuu ambao kwa muda sasa umekuwa katika mvutano mkubwa wa kisiasa ambao ulikuwa haujawahi kushuhudiwa katika muongo mmoja uliopita, umeonya kuendesha mgomo mkubwa na maandamano kuhusiana na suala hilo.

Baada ya kufanyika kura ya maoni ya kutaka kujitenga eneo hilo hapo tarehe Mosi mwezi huu, serikali kuu ya Uhispania ilitangaza kusimamisha mamlaka ya viongozi waCatalonia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.