Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Madrid yatumia ibara ya 155 kwa kufuta Serikali ya Catalonia

Katika hotuba kwa vyombo vya habari baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri, Waziri Mkuu wa Uhispania,Mariano Rajoy, amesema amelazimika kutumia ibara ya 155 ya Katiba, ambayo inaweka Catalonia chini ya mamlaka ya serikali kuu ya Madrid.

Waziri Mkuu Mariano Rajoy wakati wa hotuba yake baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri.
Waziri Mkuu Mariano Rajoy wakati wa hotuba yake baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri. REUTERS/Juan Carlos Hidalgo/Pool
Matangazo ya kibiashara

Mariano Rajoy amesema anataka uchaguzi kwa eneo hilo ufanyika ndani ya miezi sita "tutakapopata uhalali wa taasisi". Hatimaye, serikali itaomba bunge la Seneti kuidhinisha azimio la kufukuzwa rais wa Catalonia, Carles Puigdemont, ambaye anatazamia kuhutubia wananchi wa eneo hilo saa 19 usiku saa za kimataifa.

Katika taarifa ya yenye maelezo mengi baada yakikao cha Baraza la Mawaziri, Mariano Rajoy alitoa matangazo kadhaa muhimu.

Kwanza, serikali ya Madrid imetumia ibara ya 155 ya Katiba ya 1978, ambayo haijatumika kamwe katika historia ya nchi hiyo Ibara hiyo inaweka kwa muda Catalonia chini ya usimamizi wa serikali ya kitaifa. Mtazamo wa wanaharakati wa Cataloni "umemlazimu" Rajoy kutumia, "dhidi ya matakwa yetu na nia yetu," kwa ibara hii.

Pili, "tutaomba Bunge la Seneti kuipa idhni serikali kuchukua uamuzi wa kumtimua Rais wa Catalonia, Carles Puigdemont, Makamu wake wa rais Oriol Junqueras na Manaibu wake wasaidizi.

Mariano Rajoy anataka kuuchaguzi ufanyike ndani ya "kipindi kisichozidi miezi sitamiezi sita", mara tu"uhalali wa kitaasisi" utakua umerejeshwa.

Bw Rajoy amesema ibara ya 155 inatumika tu katika hali ya kipekee.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.