Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Mvutano waendelea kati ya Madrid na Catalonia kabla ya muda wa mwisho kumalizika

Muda wa mwisho uliyotolewa na serikali kuu ya Uhispania kwa rais wa Catalonia kuweka wazi tangazao lake kuhusu uhuru wa jimbo hilo unamalizika Alhamisi hii Oktoba 19 saa 10 kamili asubuhi.

Mashabiki walitumia fursa ya mechi ya Ligi ya Mabingwa ya FC Barcelona siku ya Jumatano Oktoba 18 ili kuonyesha uungwaji wao mkono kwa uhuru wa Catalonia.
Mashabiki walitumia fursa ya mechi ya Ligi ya Mabingwa ya FC Barcelona siku ya Jumatano Oktoba 18 ili kuonyesha uungwaji wao mkono kwa uhuru wa Catalonia. REUTERS/Albert Gea
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano serikali kuu ya Uhispania imetishia kuchukua hatua za kufutilia mbali utawala wa Catalonia ikiwa kiongozi wake hataachana na hatua za kutafua uhuru. Hali ya sintofahamu inatarajiwa kushuhudiwa nchini Uhispania. Rais wa Catalonia Carles Puigdemont ametishia kuvunja bunge la Catalonia endapo serikali ya Mariano Rajoy itatumia Ibara ya 155 ya Katiba.

Carles Puigdemont alipewa muda hadi Alhamisi hii Oktoba 19,saa 10 kamili asubuhi, kufuta waziwazi tangazo la uhuru. Ikiwa rais wa Catalonia hatofuata maelekezo ya serikali ya Uhispania, "atasababisha matumizi ya Ibara ya 155 ya Katiba" ambayo inaruhusu kukufuta utawala wa jimbo la Catalonia na kurudi chini ya mamlaka ya serikali kuu ya uhispania.

Naibu Waziri Mkuu wa Uhispania Soraya Sáenz de Santamaría alitoa onyo siku moja moja kabla ya siku aliyopewa Carles Puigdemont, kumalizika.

Serikali ya Catalonia imesisitiza kuwa haiwezi kutekeleza matakwa ya Madrid baada ya kura iliyokumbwa na utata ya Catalonia.

Kumekuwa na maandamano kupinga kuzuiwa kwa viongozi wa vugugu la Catalonia.

Jordi Sánchez na Jordi Cuixart wanazuiliwa huku wakichunguzwa kwa uhaini, hatua ambayo upande ambao unataka uhuru unaiona kuwa iliochochewa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.