Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Mariano Rajoy amtahadharisha rais wa Catalonia

Waziri Mkuu wa Uhispania ametoa muda hadi Jumatatu ya wiki ijayo kuwa kiongozi wa Catalonia awe amethibitisha kwamba alitangaza uhuru wa jimbo hilo au la.

Mwanaharakati wa uhuru wa Catalonia mbele ya makao makuu ya Tume ya Ulaya huko Brussels, Oktoba 2. 2017, siku moja baada ya kura ya maoni Catalonia.
Mwanaharakati wa uhuru wa Catalonia mbele ya makao makuu ya Tume ya Ulaya huko Brussels, Oktoba 2. 2017, siku moja baada ya kura ya maoni Catalonia. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake mbele ya Bunge la Catalonia ameitaka serikali ya Catalonia kuwa hadi siku ya Alhamisi ijayo iwe imerejelea hatua yake na kurudi katika sheria. Umoja wa Ulaya unafuatilia mgogoro kwa wasiwasi mkubwa. Tume ya Ulaya imesem ainaunga mkono msimamo wa serikali kuu ya Uhispania.

Hata hivyo baadhi ya maafisa wakuu wa Ulaya wamesema kuwa hakutakua na uingiliaji wowote katika sheria au katiba ya nchi ya Uhispania, huku wakiongeza kuwa vitisho kutoka pande zote havina maana yoyote wakati huu nchi yaUhispania, kinachohitajika ni kuketi pamoja kwa lengo la kupatia ufumbuzi mgogoro huo, wamesema maafisa wa hao wakuu wa Ulaya.

Pia maafisa hao wamebaini kwamba hakutakua na usuluhishi kutoka Ulaya kama kweli pande zote mbili hazitoafikiana kwa hilo.

Wakati huo huo viongozi kadhaa wa Ulaya wamekua wakiwasiliana na Waziri mkuu wa Uhispania tangu siku ya Jumatano wiki hii wakisem akuwa wanamuunga mkono kwa msimamo wake.

Katika hali ya kukabiliana na uamuzi wa kiongozi wa Catalonia, serikali ya kuu ya Uhispania imechukua hatua. Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy ametishia kutumia Ibara ya 155 ya Katiba ili kudhibiti jimbo la Catalonia ikiwa Carles Puigdemont hatofuta uamuzi wake wa kutangaza uhuru wa jimbo hilo. Wahispania wengi anasema msimamo wa serikali kuu ya Uhispania unakua umechelewa sana, ungelichukuliwa kabla.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.