Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Mvutano mkubwa waendelea kuhusu uhuru wa Catalonia

Catalonia inakabiliwa na shinikizo kubwa kabla ya hotuba muhimu kuhusu uhuru wa eneo hilo inayotarajiwa kutolewa Jumanne hii jioni na kiongozi wa eneo hilo mbele ya bunge la Catalonia.

Mvutano unaendelea uhispania kabla ya kikao cha bunge cha Jumanne 1Oktoba 10, ambapo Carles Puigdemont, kiongozi wa Catalonia anatarajia kutangaza uhuru wa eneo hilo.
Mvutano unaendelea uhispania kabla ya kikao cha bunge cha Jumanne 1Oktoba 10, ambapo Carles Puigdemont, kiongozi wa Catalonia anatarajia kutangaza uhuru wa eneo hilo. Catalan Goverment/Jordi Bedmar Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont anatishi kutangaza uhuru wa eneo hilo Jumanne hii Oktoba. Luna hatari ya hotuba hii kuchohea mgogoro wa kisiasa ambao unaendelea kuathiri nchi ya Uhispani tangu kurejesha demokrasia nchini humo.

Mpaka sasa wananchi wa uhispania na nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Ulaya wanasubiri kuona iwapo Carles Puigdemont atangaza uhuru wa Catalonia. Mchakato wa kutangaza uhuru wa eneo la Catalonia unaendelea licha ya kiongozi wa eneo hilo kuomba hivi karibuni "usuluhishi wa kimataifa".

Madai Bw. Puigdemont hayajakubaliwa na serikali, ambayo imekataa katu katu kuchukuliwa sawa na Carles Puigdemont, kwenye taasisi za Ulaya. Kwa hivyo anaweza kuamua kutangaza uhuru "kiishara," na utekelezaji wake kuchelewa, ili asipoteze msimamo wake na kuacha nafasi kwa majadiliano.

Maandamano makubwa kwa ajili ya umoja wa Uhispania, ambao ulikusanya karibu watu 500,000 walioingia katika mitaa ya Barcelona siku ya Jumapili, maandamano ambayo yaliwapa nguvu wale wanaopinga kujitenga kwa eneo hilo. Kamwe maandamano hayo hayakufanyika katika mji mkuu wa Catalonia.

Serikali kuu ya Uhispania tayari imetangaza kwamba Kama Carles Puigdemont atatangaza mbele ya Bunge la Barcelona uhuru wa Catalonia haitasita kutumia Ibara 155 ya Katiba, ambayoinaruhusu serikali kuu kufuta uhuru wa eneo lolote kama umoja wa nchi utakua hatarini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.