Pata taarifa kuu
UHISPANIA

Kiongozi wa Catalonia atoa wito wa upinzani wa kidemokrasia dhidi ya Madrid

Kiongozi wa eneo la Katalonia lililojitangazia uhuru kutoka kwa Uhispania ametoa wito wa kuweka upinzani wa kidemokrasia katika utawala wa moja kwa moja uliowekwa na serikali kuu katika eneo hilo baada ya bunge lake kujitangazia uhuru .

Kiongozi wa eneo la Catalonia lililojitenga na Uhispania Carles Puigdemont
Kiongozi wa eneo la Catalonia lililojitenga na Uhispania Carles Puigdemont REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Carles Puigdemont amesema katika taarifa iliyorushwa kupitia televisheni kuwa Njia bora ya kutetea yale waliyofanikisha hadi sasa ni upinzani wa kidemokrasia dhidi ya matumizi ya kifungu cha 155 cha katiba kinachoipa Madrid mamlaka ya kutawala eneo hilo, na kuongeza kwamba yeye na timu yake wataendelea kufanya kazi "kujenga nchi huru."

Uhispania inabaki kuwa katika mvutano mkali wakati huu ikikabiliana na mgogoro mbaya zaidi wa kikatiba katika historia yake ya kisasa, uliochochewa na kura ya maoni ya Oktoba 1 ambayo ilitajwa kuwa kinyume cha sheria.

Wabunge wa Katalonia siku ya Ijumaa walipitisha azimio la kujitenga kwa kura 70 kati ya 135 katika bunge la kikanda, na kutangaza eneo la Katalonia kuwa Jamhuri.

Wabunge wa upinzani walikataa hata kupiga kura na kutoka nje ya bunge wakiwa wamechukia.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.