Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Carles Puigdemont : Siombi hifadhi ya ukimbizi Ubelgiji

Aliyekuwa rais wa Catalonia, Carles Puigdemont, ambaye yuko nchini Ubelgiji tangu Jumatatu hii Oktoba 30, amekutana Jumanne hii mchana na waandishi wa habari mjini Brussels.

Kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont katika mkutano na waandishi wa habari, Brussels tarehe 31 Oktoba 2017.
Kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont katika mkutano na waandishi wa habari, Brussels tarehe 31 Oktoba 2017. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Bw. Puigdemont amesema kuwa anashtumiwa kuanzisha uasi dhidi ya serikali kuu ya Uhispania, hana nia ya kuomba hifadhi yoyote ya ukimbizi nchini Ubelgiji na ataendelea na majukumu yake dhidi ya vyombo vya sheria vya nchi yake, lakini ameomba kuepo na "dhamana". Pia amese akuwa ataheshimu matokeo ya uchaguzi wa Desemba 21 na aetoa wito wa "kupunguza" kasi katika mchakato wa uhuru wa eneo la Catalonia ili kuzuia machafuko.

Bw. Carles Puigdemont aliwasili Brussels siku ya Jumatatu ya 30 Oktoba na viongozi wengine watano wa Catalonia. Baada ya masaa 24 ya ukimya, na kupelekea uvumi kuchukua nafasi ya kuligawa taifa la Uhispania, Bw Puigdemont alizungmza na waandishi wa habari katika jengo la Club Press mjini Brussels katika lugha tatu: Kikatalonia, Kihispania na Kifaransa.

Carles Puigdemont alianza kukumbusha sababu zilizopelekea anakwenda Brussels. Amebaini kwamba, kutokana na mwenendo wa serikali ya Uhispania, Ijumaa, Oktoba 27, "mazungumzo yenye utulivu na kidiplomasia hayawezekani." Amelaani "sera ya ukandamizaji na sio ya majadiliano."

Carles Puigdemont alitetea mshikamano wa hatua yake na kusisitiza mara kadhaa kukataa kwake kwa hatua yoyote ya vurugu. "Tumelazimika kwenda sambamba na mpango wetu wa kazi zetu ili kuepuka vurugu" na "kama tabia hii ina lengo la mchakato wa Catalonia kuwa taifa huru, wangelipaswa kufahamu kuwa wakati umewadia wa Catalonia kujitawala na kuwa huru, ameongeza Bw. Puigdemont.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.