Pata taarifa kuu
UFARANSA-EU-USHIRIKIANO

Emmanuel Macron kuonyesha mipango yake kuhusu Umoja wa Ulaya

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kutoa hutuba hii leo, yenye lengo la kuonyesha mtazamo wake kuhusu Umoja wa Ulaya lakini ia kugusia mchango na siasa za Ujerumani katika Umoja huo.

Ni Jumanne hii alasiri katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sorbonne mjini Paris ambapo Rais Emmanuel Macron ataonyesha mpango wake kuhusu Umoja wa Ulaya.
Ni Jumanne hii alasiri katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sorbonne mjini Paris ambapo Rais Emmanuel Macron ataonyesha mpango wake kuhusu Umoja wa Ulaya. AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati akiingia madarakani Rais Macron aliahidi kuimarisha taasisi za ukanda wa Euro pamoja na kuimarisha Uhusiano wa kidiplomasia na Umoja wa Ulaya wakati ambapo Uingereza inaelekea kukamilisha mchakato wa kujiondoa kwenye Umoja huo

Macron amefurahishwa na Mpango wa Kansela wa Ujerumani wa kufanya marekebisho katika ajenda mbalimbali, mabadiliko ambayo yanajumuisha mipango ya nafasi mpya ya waziri wa fedha, bajeti na bunge kwa wanachama 19 wa Umoja huo

Mipango ya Rais Macron imechagizwa na uchaguzi wa Ujerumani uliofanyika mwishoni mwa juma hili,unaopelekea kuundwa kwa serikali mpya inayojumuisha chama cha Free Democratic Party (FDP),chama ambacho kiongozi wake anaunga mkono ajenda ya Macron ya kufanyika kwa mabadiliko katika Umoja wa ulaya EU

Aidha, Macron atatumia hotuba hiyo atakayoitoa katika chuo kikuu cha Sorbonne kuzungumzia mabadiliko chanya katika taasisi za umma, juhudi za kuimarisha Umoja wa Ulaya EU, mipango yake katika kuboresha huduma za kiteknolojia ,Ulinzi pamoja na sekta za Nishati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.