Pata taarifa kuu
UFARANSA-LIBYA-WAHAMIAJI

Macron: Libya inatakiwa kuwakabili wahamiaji haramu

Akiwa ziarani Orleans, Alhamisi, Julai 27, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alielezea sera ya uhamiaji ya Ufaransa katika miaka yake mitano ya uongozi wa nchi pamoja na tofauti ya wazi kati ya wakimbizi wa kisiasa na wahamiaji wa kiuchumi.

Rais Emmanuel Macron, Alhamisi, Julai 27 Orleans, ambapoalitoa sera yake kabambe ya kushughulikia mgogoro wa wahamiaji.
Rais Emmanuel Macron, Alhamisi, Julai 27 Orleans, ambapoalitoa sera yake kabambe ya kushughulikia mgogoro wa wahamiaji. Michel Euler / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron anataka kutafautisha wahamiaji wa kiuchumi na wakimbizi. Anataka kuongeza kasi ya taratibu ya kuomba hifadhi ya ukimbizi. Rais wa Ufaransa amesema anataka kurudisha muda wa miezi 6 badala ya mwaka hadi miezi 18 leo nchini Ufaransa.

Maombi ya hifadhi ya ukimbizi yatashughulikiwa nje ya ardhi ya Ufaransa katika vituo vya uchunguzi. Wahamiaji wengi wanaingia nchini Italia wakielekea Ulaya, na wengi wanatokea bara la Afrika. Mikakati lazima ichukuliwe katika "Nchi zinazojulikana" kutokea wahamiaji.

Rais Emmanuel Macron amezitaja nchi za Niger, Chad na Libya.

Rais Emmanuel Macron amesisitiza, akitaka msaada wa Ulaya, ingawa baadhi ya nchi za Ulaya zinasita kutekeleza ahadi zao.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ametoa mapendekezo ya kuweka vituo nchini Libya ili kutekeleza mahitaji ya raia wanaomba hifadhi nje ya taifa hilo.

Hatua hiyo ni kufuatia Italia kuonyesha mashaka katika jambo hilo.

Macron amesema kuwa mradi huo utaanza kutekelezwa ndani ya miezi miwili ijayo.

Lakini Waziri mkuu wa Italia, Paolo Gentiloni, amesema kuwa tatizo la ukimbizi haliwezi kutatuliwa kwa njia ya kuwaondoa nchini humo.

“Umoja Ulaya unapaswa kuchukua hatua ambazo zitaipatia uwezo Libya kuleta hali ya Amani” , amesema Paolo Gentiloni, huku akiongeza kuwa wiki ijayo wanatarajia kuwasilisha muswada bungeni utakaowapa mamlaka Italia kutumia vyombo vya majini kukabiliana na wahalifu ndani ya Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.