Pata taarifa kuu
UFARANSA-AFRIKA-WAKIMBIZI-UGAIDI

Rais wa Ufaransa kupambana na ugaidi na uhamiaji Afrika

Siku ya Jumanne, Agosti 29, rais wa Ufaransa alielezea baadhi ya vipengele vikuu vya sera yake ya kigeni wakati wa hotuba yake ya jadi kwa mabalozi 170 wa Ufaransa duniani.

Emmanuel Macron na wajumbe wa Baraza lake kwa Afrika, Humanne Agosti 29, 2017 Élysée.
Emmanuel Macron na wajumbe wa Baraza lake kwa Afrika, Humanne Agosti 29, 2017 Élysée. REUTERS/Yoan Valat/Pool
Matangazo ya kibiashara

Akiitaja Afrika kuwa "bara la siku zijazo", Emmanuel Macron aliweka vipaumbele vyake: kupambana dhidi ya ugaidi na kupambana na uhamiaji haramu.

Rais wa Ufaransa alirejelea vipaumbele vikuu viwili vya sera yake ya nje lakini pia sera ya Afrika, ambayo ni kupambana dhidi ya ugaidi na kupunguza kiwango cha uhamiaji haramu.

Kipaumbele cha kwanza: vita dhidi ya "ugaidi wa Kiislam"

Kuhusu ugaidi, kwanza, Emmanuel Macron alisema kuwa kuna ulazim awa kuimarisha jitihada za kidiplomasia za Ufaransa nchini Syria na Iraq, bila shaka, lakini pia nchini Libya na katika ukanda wa Sahel, vituo viwili vya ugaidi katika la bara la Afrika. "Kpambana dhidi ya ugaidi wa Kiislamu" ni "kipaumbele cha kwanza" kwenye azma yake ya kidiplomasia, alisema rais wa Ufaransa.

"Ndiyo, ninazungumzia juu ya ugaidi wa Kiislamu na nakubali kikamilifu matumizi ya kivumishi hiki," Bw Macron alisisitiza. "Kwa maana hakuna chochote kile kitakuwa cha ajabu kuliko kukataa uhusiano kati ya vitendo vya kigaidi tunavyoshuhudia na kusoma imani ya msingi na ya kisiasa wa Uislam fulani.

Wakati huo huo Emmanuel Macron alisema wanataka kuhusisha mbinu ya usalama na maendeleo ya kiuchumi ya maeneo haya. Mfano huko Mali, na uamuzi wa jeshi la Ufaransa kwa upande mmoja lakini hautoshi, "lazima tufanye zaidi," aalisema rais wa Ufaransa kuhusu kuanzishwa kwa makubaliano ya amani, lakini pia maendeleo . Kwa hivyo alitangaza siku ya Jumanne asubuhi uteuzi wa mjumbe maalum wa usalama na maendeleo ya Sahel bila kutoa maelezo zaidi.

Balozi anayehusika na masuala ya uhamiaji

Kipaumbele kingine ni "mgogoro wa wahamiaji", kama alivyouita Emmanuel Macron. "Kuwapokea wahamiaji ni wajibu wa kibinadamu," alisema rais wa Ufaransa, bila kupendekeza ufumbuzi wowote.

Hata hivyo, alitangaza uteuzi wa balozi anayehusika na kuratibu mazungumzo ya uhamiaji kati ya Ufaransa, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika.

Kwa ujumla, hotuba hii ya Jumanne asubuhi ilitoa ufafanuzi mdogo juu ya suala hili. Badala yake, itasaidia kuchunguza matendo ya serikali ya Ufaransa na kurejelea matangazo ambayo tayari awali yalipitishwa.

Emmanuel Macron, hata hivyo, alitangaza kuzuru Ouagadougou. Ziara katika mji mkuu wa Burkina Faso, ambapo tarehe haijawekwa wazi, lakini ziara ambayo itampa fursa ya kuendelea kutoa maono yake ya siasa za Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.