Pata taarifa kuu
UFARANSA-MACRON-SIASA

Emmanuel Macron kulihutubia bunge mjini Versailles

Miezi michahe baada ya kuchaguliwa, rais wa Ufaransa anatazamiwa kutoa zera yake Jumatatu hii Julai 3 mbele ya Bunge la Ufaransa mjini Versailles, mchakato wa kipekee katika hatua hii ya muhula wa miaka mitano ijayo.

Emmanuel Macron kwa mara ya kwanza atalihutubia bunge, katika mwanzo mwa muhula wake.
Emmanuel Macron kwa mara ya kwanza atalihutubia bunge, katika mwanzo mwa muhula wake. REUTERS/Thibault Camus/Pool
Matangazo ya kibiashara

Rais Macron atatoa idadi kadhaa ya mipango aliyotangaza wakati wa kampeni za urais na kufafanua ndoto yake kwa kipindi cha miaka mitano.

Hii itakua ni mara ya kwanza kwa rais Macron kulihutubia Bunge miezi kadhaa baada ya kuchaguliwa rais wa Ufaransa. Tofauti na watangulizi wake wawili Nicolas Sarkozy na Francois Hollande ambao walikua wakitoa hotuba za mara kwa mara, Emmanuel Macron aliamua kutpfanya hivyo.

Tofauti na watangulizi wake, Rais Macron amechagua kutoshiriki mahojiano kwenye televisheni ya Julai 14, taasisi ya vyombo vya habari iliyozinduliwa rasmi miaka arobaini iliyopita na Valery Giscard d'Estaing.

Itakuwa ni mara ya tatu chini ya awamu ya Tano rais analihutubia mabaraza mawili ya Bunge, mpango uliowezekana, tangu kupitishwa kwa sheria ya Julai 23, 2008 inayoruhusu marais kupewa nafasi ya kuzungumza mbele ya Bunge. Mara ya kwanza ilikuwa tarehe 22 June mwaka 2009 wakati Nicolas Sarkozy alipotangaza kuchukuliwa kwa hatua kadhaa, hasa kushughulikia mgogoro wa kiuchumi, na mara pili ilikua tarehe 16 Novemba 2015, wakati François Hollande alipowataka wananchi kuungana katika mapambano dhidi ya ugaidi baada ya mashambulizi yalitokea mapema siku tatu katika mji wa Paris. Hata hivyo ni mara ya kwanza kwa Rais kukutana na wabunge katika mwanzo wa muhula wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.