Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA

François de Rugy achaguliwa Spika wa Bunge la Ufaransa

François de Rugy, mwanamazingira wa zamani aliyejiunga na chama cha Republique en marche, alichaguliwa siku ya Jumanne Juni 27 Spika wa kumi na tatu wa Bunge la awamu ya Tano nchini Ufaransa.

François de Rugy, wakati wa vikao vya uzinduzi wa bunge la 15 nchini Ufaransa, Juni 27, 2017.
François de Rugy, wakati wa vikao vya uzinduzi wa bunge la 15 nchini Ufaransa, Juni 27, 2017. Patrick KOVARIK / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kulikuwa na wapiga kura 567. Kura 24 zilikua tupu au ziliharibiwa. Kulikuwa hasa na kura 543. Kura zilizokua zinahitajika kwa kupitishwa kwa Spika wa Bunge zilikua 272. François de Rugy alipata kura 353, " alitangaza muda mfupi kabla ya saa 11 jioni katika ukumbi wa mikutano ya Bunge mbunge mwenye umri mkubwa kwa wabunge wote, Bernard Brochand kutoka chama cha LR, ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho. Wabunge walikaribisha kuchaguliwa kwa François de Rugy.

Wagombea wengine wanne walioshiriki kinyang'anyiro hiki ni pamoja na Jean-Charles Taugourdeau kutoka chama cha Republican ambae alipata kura 94, akiongoza dhidi ya Laurence Dumont kutoka chama cha Nouvelle gauche (zamani kikiitwa PS 32). Alipata kura 32. Caroline Fia kutoka chama cha La France insoumise, ambaye alikua aliungwa mkono na kundi la mrengo wa kulia la chama cha Democratic na Republican, alipata kura 30, huku Laure de la Raudière kutoka chama cha LR, UDI na wagombea binafsi wakipata kura 4.

François de Rugy, aliteuliwa saa chache na kundi la LREM, ambalo peke yake lina idadi kubwa ya wabunge ambao ni sawa na 308, liliungwa mkono chama cha MoDem.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.