Pata taarifa kuu
UINGEREZA-USALAMA-MAUAJI

Ulinzi waimarishwa Manchester

Kwa kuonyesha mshikamano wa watu wa Manchester na waathirika wa shambulio lililotokea baada ya tamasha la muziki siku ya Jumatatu usiku, meya wa mji huo aliwataka wakazi wa mji huo kukesha Jumanne usiku mbele ya makao makuu ya manispaa ya jiji la Manchester. Nchini kote Uingereza Bendera zimepandishwa nusu mlingoti.

Watu kadhaa wakishikilia mabango yalioandikwa "I Love MCR" (Naipenda Manchester).
Watu kadhaa wakishikilia mabango yalioandikwa "I Love MCR" (Naipenda Manchester). REUTERS/Darren Staples
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo polisi ya Manchester imeimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mji huo.

Katika siku ya jana sherehe mamia kwa maelfu ya watu walikusanyka katika eneo kulikotokea shambulio hilo kwa kuonyesha umoja na mshikamano nakama kitendo cha kufutilia mbali na kupinga ugaidi.

Shambulio hilo lililotokea baada ya tamasha la mwanamuziki Ariana Grand kutoka Marekani.

Makao makuu ya jiji la Manchester yalifurikwa na watu kutoka tabaka mbalimbali ikiwa ni pamoja na wachungaji wa kanisa la Anglikana, Waislamu, vijana wa Kiyahudi, wanaume kwa wanawake wa umri mbalimbali walikusanyika, baadhi yao wakishikilia mabango yalioandikwa upendo kwa kila mtu, chuki haina maana yoyote.

"Tutashinda magaidi katika utofauti wetu," alisema Meya wa jiji la Manchester Eddy Newman, aliyechukua nafasi ya kushukuru huduma za idara za dharura.

Wakati huo Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema Uingereza itasambaza wanajeshi kwa ajili ya kulinda maeneo muhimu na kwenye matukio mbalimbali, kufuatia shambulio la kigaidi lililotokea katika mji wa Manchester na kusababisha vifo vya watu 22.

Theresa May amesema ukadiriaji unaofanywa juu ya kitisho cha ugaidi kinachoikabili nchi hiyo, umeongezwa kwa kiwango kikubwa.

Waziri mkuu wa Uingereza amesisitiza kuwa kuna uwezekano wa baadhi ya raia wa Uingereza walishirikiana na magaidi kwa kutekeleza shambulio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.