Pata taarifa kuu
EU-UINGEREZA

EU kuchapisha rasimu ya mpango wa Uingereza kujitoa

Rais wa baraza la umoja wa Ulaya Donald Tusk anatarajia kutoa rasimu ya awamu kuhusu mpangilio wa namna umoja wa Ulaya umepanga kufanya majadiliano na Uingereza kujitoa kwenye umoja huo.

Bendera ya umoja wa Ulaya ikipepea kwenye mnara wa London.
Bendera ya umoja wa Ulaya ikipepea kwenye mnara wa London. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mapendekezo haya ya rais Tusk yatatumwa kwa nchi zote 27 wanachama wa umoja wa Ulaya ili waipitie rasimu hiyo.

Nchi wanachama kupitia rasimu hiyo watapendekeza namna bora nyingine ya kusimamia mazungumzo hayo ambayo yatadumu kwa miaka miwili hadi nchi ya Uingereza itakapokuwa imekamilisha kujiondoa kwake.

Wakuu wa nchi za Ulaya wanataka kwanza nchi ya Uingereza ikubali masharti ya kujiondoa kwake kabla ya kuanza kwa mazungumzo yatakayotoa mustakabali wa uhusiano wa baadae na umoja huo.

Uingereza yenyewe inatoa wito wa kufanyika mazungumzo yanayoenda sambamba bila kubagua ikiwa imekubali masharti ya kujitoa kwake au la.

Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May. 29 Machi, 2017
Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May. 29 Machi, 2017 Parliament TV handout via REUTERS

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May tayari ameshaandika barua rasmi kwenye umoja huo kueleza nia yake ya kujitoa na kuanza kutekeleza mchakato wa kitengua ibara ya 50 ya mkataba wa Lisbon ulioanzisha umoja huo.

Tusk ambaye kwa sasa yuko nchini Malta kwa mazungumzo na viongozi wa vyama vya mrengo wa kati, anatarajia kutuma rasimu hiyo kwa nchi wanachama 27 Ijumaa hii.

Umoja wa Ulaya umesema utachapisha rasimu hiyo ya muongozi kwenye tovuti yake lakini kuna taarifa kuwa nchi mbili wanachama zinapinga rasimu hiyo kuchapishwa kwenye tovuti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.