Pata taarifa kuu
UTURUKI-PKK-MAPIGANO

Uturuki: Erdogan adai kuwaua waasi 3,000 wa PKK mwaka 2015

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwa mara nyingine ameahidi Alhamisi hii katika hotuba ya kuwatakia Mwaka Mpya raia wake, kuwa ameliangamiza kundi la waasi wa Kikurdi wa PKK, na kujisifu kuwa aliwaua waasi 3,000 wa kundi hilo mwaka 2015.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, wakati wa hotuba yake katika ukumbi wa Ikulu ya rais jijini Ankara, 26 Aprili 2015.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, wakati wa hotuba yake katika ukumbi wa Ikulu ya rais jijini Ankara, 26 Aprili 2015. REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

"Jamhuri ya Uturuki ina nafasi na dhamira ya kulishinda kundi la kigaidi la PKK. Vikosi vyetu vya usalama vinawaangamiza magaidi kwa kila sentimita ya milima na mijini na vitaendelea kufanya hivyo", Bw Erdogan amesema katika ujumbe wake wa kijadi uliyorushwa hewani kwenye runinga Alhamisi hii Desemba 31.

"Serikali yetu imejikubalisha kikamilifu kuendelea na mapambano yake dhidi ya ugaidi", Ofisi ya Waziri mkuu Ahmet Davutoglu imesisitiza Alhamisi hii, katika taarifa iliyotolewa wakati wa kuhitimisha mkutano mpya wa usalama.

Baada ya zaidi ya miaka miwili ya mapigano, mapigano yalianza upya katika majira ya joto kati ya Ankara na waasi wa kundi la PKK, na hivyo kusababisha kuvunjika kwa mazungumzo ya amani mwaka 2012 ili kumaliza mgogoro uliosababisha vifo vya watu zaidi 40,000 tangu mwaka 1984.

"Karibu magaidi 3,100 waliangamizwa katika operesheni ziliofanywa mwaka 2015 katika ardhi yetu na nje ya nchi", Erdogan amesema Alhamisi hii, akimaanisha mashambulizi ya jeshi dhidi ya kundi la PKK nchini Uturuki au kaskazini mwa Iraq.

Maafisa wa polisi na askari zaidi ya 200 waliuawa katika mapigano hayo, ikiwa ni pamoja na raia wa kawaida, rais Erdogan amesikitishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.