Pata taarifa kuu
UFARANSA-UBELGIJI-SHAMBULIO-USALAMA

Shambulio Paris: mtuhumiwa wa tisa ashtakiwa Ubelgiji

Mtuhumiwa wa tisa amekamatwa na kushtakiwa knchini Ubelgiji kuhusiana na mashambulizi yaliotokea mjini Paris, nchini Ufaransa, Ofisi ya mashataka nchini Ubelgiji imeliambia Alhamisi hii shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Mwili wa mtu aliyeuawa ukiondolewa chini ya vifusi baada ya shambulio ambapo Hasna Aitboulahcen na Abdelhamid Abaaoud waliuawa Novemba 18, 2015 katika mji wa Saint-Denis, karibu na mji wa Paris.
Mwili wa mtu aliyeuawa ukiondolewa chini ya vifusi baada ya shambulio ambapo Hasna Aitboulahcen na Abdelhamid Abaaoud waliuawa Novemba 18, 2015 katika mji wa Saint-Denis, karibu na mji wa Paris. AFP/AFP/
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya mashtaka imethibitisha kwamba mtuhumiwa huyu alikua akiwasiliana na Abdelhamid Abaaoud anayetuhumiwa kuandaa mashambulizi hayo.

Baada ya mashambulizi ya kigaidi ya mjini Paris na kabla ya mashambulizi na Saint-Denis mshukiwa huyo aliye kamatwa aliwasiliana mara kadhaa na Hasna Aitboulahcen.

Hasna Aitboulahcen na Abdelhamid Abaaoud waliuawa katika mashambulizi hao, msemaji wa Ofisi ya mashitaka, Eric Van der Sypt, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.