Ufaransa: mshambuliaji wa tatu wa kujitoa mhanga atambuliwa
Karibu mwezi mmoja baada ya mashambulizi ya jijini Paris, Novemba 13, 2015, polisi hatimaye imemtambua mshambuliaji wa mwisho wa kujitoa mhanga ambaye alijilipua katika ukumbi wa Bataclan, karibu na eneo la Jamhuri. Ni mkazi wa Strasbourg, mwenye umri wa miaka 23, anayeitwa Mohamed Fouad Aggad.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kama yule ambaye aliyeandaa mashambulizi, raia wa Ubelgiji, Abdelhamid Abaaoud, Mohamed Fouad Aggad alikua aanajulina vema kwa sababu alijidhihirisha mwenyewe kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook akiweka picha yake alipokua nchini Syria, hasa ile yenye sifa mbaya akivaa kichwani utepe ambapo mbele ya utepe huo kulikua na bendera ya kundi la Islamic State.
Foued est le 3e kamikaze du Bataclan identifié. En 2014, il avait posté cette photo de lui sur Facebook. pic.twitter.com/u19WT9xH73
— David Thomson (@_DavidThomson) December 9, 2015
Ni mtu ambaye alitambuliwa vema na licha ya hao aliweza pia kurudi Ufaransa bila hata hivyo Idara ya ujasusi kujua.
Mohamed Fouad Aggad alienda Syria na kaka yake na marafiki zake kumi kutoka eneo maarufu la Meinau alipokua akiishi katika mji wa Strasbourg mwishoni mwa mwezi 2013. Marafiki zake waliarudi mwezi Februari 2014, hasa baada ya kifo cha wenazo wawili katika mapambano na waasi wengine. Waliporudi walikamatwa.
Mohamed Fouad Aggad aaliamua kubaki nchini Syria. Taarifa za mwisho, zinabaini kwamba alikua akipigania nchini Iraq. Mke wake, mabaye ni raia wa Ufaransa, bado ypo Syria, na alijifungua hivi karibuni.
Ni mpiganaji wa sita wa kiislamu ambaye ametambuliwa baada ya kupoteza maisha katika mashambulizi mabaya kuwahi kutokea nchini Ufaransa kwa kipindi cha miaka mitatu.