Pata taarifa kuu
UFARANSA-URUSI-USHIRIKIANO

Ufaransa-Urusi: mipaka ya muungano dhidi kundi la IS

François Hollande amefanya ziara Alhamisi hii Novemba 26 mjini Moscow kujadili na Putin uanzishwaji wa muungano kabambe dhidi ya kundi la Islamic State. Lakini Paris na Moscow watapaswa kwanza kufafanua misimamo yao kuhusu maeneo yatakayolengwa na mustakabali wa kisiasa wa Syria.

Rais wa Ufaransa François Hollande na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin katika uwanja wa ndege wa Moscow, Desemba 6, 2014.
Rais wa Ufaransa François Hollande na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin katika uwanja wa ndege wa Moscow, Desemba 6, 2014. AFP/Alain Jocard
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kuibuka kwa uhasama kufuatia kuangushwa kwa ndege ya Urusi nchini Uturuki, Moscow Novemba 26, ilisema iko tayari kushiriki katika muungano wa kijeshi wa pamoja kwa ajili ya kupanga mashambulizi dhidi ya kundi la Islamic State.

"Ili kuendeleza muungano wa pamoja, inatubidi tuwe na malengo ya pamoja", Wizara ya ulinzi ya Ufaransa imebaini. Kwa maneno mengine, Urusi inapaswa kusitisha mashambulizi yake dhidi ya makundi ya wanaharakati wa upinzani wa wenye msimamo wa wastani nchini Syria. Kwa sababu 50% hadi 60% ya mashambulizi ya Urusi hayagusi Daech wala Jabat al-Nosra Front,Wizara hiyo imeongeza.

Jambo la pili: Suala la Assad na utawala wa Syria. "Hatuwezi kufanya safu ya harakati kinyume na wanajihadi bila dhamana juu ya baada ya Bashar", vyanzo vya kijeshi vimebaini mjini Paris. "Pamoja na Warusi tunapaswa kuzungumzia kuhusu suala hili". "Ufaransa, kama Urusi, wamekumbwa na mashambulizi ya kigaidi". "Hakuna mtu anayeweka hatarini maslahi ya Urusi nchini Syria, ambayo pia hupatikana katika muundo wa nchi hii", chanzo hicho kimeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.