Pata taarifa kuu
UFARANSA-UJERUMANI-USHIRIKIANO

Hollande atazamiwa kumpokea Merkel

Baada ya kuondoka Washington ambapo amekubaliana na Barack Obama kuwa na umoja katika mapambano dhidi ya kundi la Islamic State, Rais wa Ufaransa François Hollande anatazamiwa kumpokea leo Jumatano kansela wa Ujerumani Angela Merkel kabla ya kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow Alhamisi wiki hii.

Rais wa Ufaransa  François Hollande (kushoto) na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Oktoba 27, 2015 katikaIkulu ya Elysee mjini Paris.
Rais wa Ufaransa François Hollande (kushoto) na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Oktoba 27, 2015 katikaIkulu ya Elysee mjini Paris. STEPHANE DE SAKUTIN/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Lakini "mshikamano mkubwa" dhidi ya kundi la Islamic State haujaanza kutekelezwa kwa sababu mbali ya nia ya nchi za Magharibi kwa kufanya vita dhidi ya kundi hilo la kijihadi lililokiri kuhusika na mashambulizi ya jijini Paris, tofauti na Urusi kuhusu Syria bado zinaendelea.

"Sisi wote ni wa Ufaransa", amesema Obama kwa Kifaransa akiambatana na rais wa Ufaransa François Hollande, katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Jumanne hii katika Ikulu ya White House.

Siku kumi na moja baada ya mashambulizi mabaya zaidi kufanyika nchini Ufaransa, Rais Obama amesema Marekani na Ufaransa "wameungana" na "wameshikamana kikamilifu" katika vita dhidi ya ugaidi.

"Tunawapenda Wafaransa", Rais Obama amesema, huku akikumbusha kwamba Ufaransa ni mshirika wa zamani wa "Marekani", akimaanisha Mapinduzi ya Marekani ya karne ya 18 ikisaidiwa na Ufaransa na Ufaransa ilikua bega kwa bega na Marekani katika mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 huku ikisema "Sisi wote ni Wamarekani."

Alhamisi wiki hii, rais wa Ufaransa François Hollande, atakutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow. Lengo ni kutafuta muungano wa kupambana na kundi la Islamic State magaidi wanaoendelea kutishia usalama wa dunia. Lakini wadadisi wanasema mazungumzo kati ya wawili hao yataishia patupu, kufuatia vita ya maneno kati ya Urusi na Uturuki iliyojitokeza baada ya ndege ya kijeshi ya Urusi kudunguliwa katika ardhi ya Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.