Pata taarifa kuu
UFARANSA-TABIA NCHI

Hollande: "bado kuna upinzani katika mkutano kuhusu tabia nchi"

Rais wa Ufaransa François Hollande amesema Jumatano wiki hii kuwa mazungumzo kwa makubaliano juu ya mkutano kuhusu tabia nchi (COP21) yalikuwa "yakiendelea vizuri" lakini "bado kuna upinzani kutoka Marekani", akisema "wakati wa maamuzi umewadia".

Rais François Hollande katika mkutano kuhusu tabia nchi katika eneo la Bourget karibu na mji wa Paris, Desemba 9, 2015.
Rais François Hollande katika mkutano kuhusu tabia nchi katika eneo la Bourget karibu na mji wa Paris, Desemba 9, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Leo hii, katika siku mbili zijazo ni wakati wa maamuzi" na sio "wakati wa utaalamu", rais wa Ufaransa amesema wakati wa utoaji wa tuzo katika Ikulu ya Elysée kwa viongozi walipambana katika masuala ya tabia nchi, kama Nicolas Hulot, mjumbe maalum wa rais kwa ulinzi wa dunia.

"tunachoomba marais na viongozi wa nchi wakuu wa nchi sio kuwa wataalamu lakini kuchukua maamuzi", Hollande amesema. "Huu ni wakati wa kupambanua", rais Hollande amesisitiza wakati ambapo mkutano unamalizika Ijumaa wiki hii.

"Bado hatujafika, tuko njia, natumaini njia sahihi, lakini tunajua kwamba bado kuna upinzani, maswali kutoka Marekani", ameongeza Hollande, bila kutaja nchi hizo "kwa kukata kuvuruga" mazungumzo.

"Sio kusaini mkataba wowote" ambayo "hautokabiliana na changamoto", Hollande ameonya.

"Kwa Ufaransa, kuna malengo kadhaa ambayo tunataka kuhifadhi", pia Hollande amebaini, akisema kwamba lengo la kwanza ilikuwa "kubaki kwenye njia ambayo itapelekea sayari kutokua na joto kwenye kiwango cha zaidi ya digrii 2 (...) hadi mwisho wa karne. "

Pamoja na ahadi zilizotolewa, "tuko juu ya kiwango cha digrii 2, hivyo umuhimu wa marekebisho ya ahadi zetu" amesema, huku akielezea kwamba marekebisho hayo ya kwanza yanapaswa kufanyika "hata kabla ya makubaliano kuanza kutekelezwa, hii inamaanisha kabla ya mwaka 2020".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.