Pata taarifa kuu
UFARANSA-AFRIKA-NISHATI

Paris yaahadi Euro bilioni 2 kwa Afrika kwa nishati mbadala

Ufaransa imeahadi Euro bilioni mbili kwa Afrika ifikapo mwaka 2020 ili kuendeleza nishati mbadala, Rais wa Ufaransa François Hollande ametangaza Jumanne hii katika mkutano na viongozi wa Afrika wakati wa mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (COP21), katika mji wa Bourget karibu na mji wa Paris.

Paris inaonyesha mfano wa kulipa "madeni kuhusu uchafuzi wa mazingira" kwa bara la Afrika.
Paris inaonyesha mfano wa kulipa "madeni kuhusu uchafuzi wa mazingira" kwa bara la Afrika. PHILIPPE WOJAZER/POOL Agencies/AFP
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa itawekeza "Euro bilioni mbili katika sekta ya nishati mbadala" barani Afrika, Rais wa Ufaransa amesema.

Itakumbukwa kwamba msaada wa Ufaransa katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi utafikia Euro bilioni 3 hadi 5 kwa mwaka ifikapo mwaka 2020, François Hollande amesisitiza kwamba "Afrika itafaidika na sehemu kubwa ya jitihada (hii)".

"Ufaransa inataka kuonyesha mfano", kuonyesha kwamba haiko tu "msaada kwa vikosi vya Afrika ambavyo vinapaswa kuimarisha usalama barani humo".

Ufaransa "inataka kusaidia kikamilifu bara la Afrika", Hollande ameendelea kusema, akijibu wito kutoka viongozi wenzake kadhaa wa Afrika.

"Afrika inakabiliwa na madhara ya ongezeko la joto duniani, wakati ambapo haihusiki kwa kusambaza gesi chafu", François Hollande pia amebaini, akisema kuwa "kuna deni la masuala ya mazingira ambalo ulimwengu unapaswa kulifidia bara la Afrika. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.