Pata taarifa kuu
TABIA NCHI-UFARANSA-HATUA

Mkutano kuhusu hali ya hewa, wito watolewa kwa kuiokoa dunia

Marais na viongozi wa serikali kutoka duniani kote wametoa Jumatatu wiki hii wito wa hatua za haraka dhidi ya ongezeko la joto duniani, lakini hali tata inayozigawanya nchi za Kaskazini na Kusini imeonekana haraka, katika mkutano kabambe ulioitishwa na Umoja wa Mataifa mjini Paris siku ya kwanza ya mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.

Ségolène Royal, Laurent Fabius, Ban Ki-moon, François Hollande na Barack Obama, Novemba 30, 2015 katika mji wa Bourget katika mkutano wa kimataifa kuhusu tabia nchi.
Ségolène Royal, Laurent Fabius, Ban Ki-moon, François Hollande na Barack Obama, Novemba 30, 2015 katika mji wa Bourget katika mkutano wa kimataifa kuhusu tabia nchi. LOIC VENANCE/POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika ufunguzi wa mkutano huo muhimu kwa dunia, viongozi 150, ikiwa ni pamoja na Baracko Obama wa Marekani, Xi Jinping wa China, Abe wa Japan, François Hollande wa Ufaransa wamesalia kimya dakika moja baada ya mashambulizi ya hivi karibuni yaliotokea katika nchi kadhaa ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na Ufaransa.

Mapambano dhidi ya ugaidi na vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi ni "changamoto mbili kubwa kimataifa ambazo tunapaswa kukabiliana nazo," François Hollande amesema katika jukwa la mkutano uliofanyika katika mji wa Bourget (kaskazini mwa Paris).

"Tunahitaji (kwa watoto wetu) sayari inayolindwa na maafa", Rais Hollande amesisitiza, akibainisha kuwa mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa (COP21) ni "tumaini kubwa ambalo tunatakiwa kuliunga mkono kwa dhati": "Tunatakiwa kuamua hapa mjini Paris kwa ajili ya hatma ya dunia. "

Mkutano unatarajiwa hadi Desemba 11 kuwa umefikia mkataba wa kwanza ya wa kimataifa katika kupunguza uzalishaji wa gesi chafu, ili kuzuia ongezeko la joto kwa kiwango cha "2 ° C ikilinganishwa na kabla ya ujio wa viwanda.

"Mkutano mkubwa wa marais na viongozi wa serikali katika jukwa na moja siku moja", umekaribishwa katika tweet na afisa wa masuala ya hali ya hewa katika Umoja wa Mataifa, Christiana Figueres.

Barack Obama, mchafuzi mkuu duniani (baada ya China), ametoa wito kwa wenzake "kukabiliana" na suala hilo, akitupilia mbali hoja kuwa mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi yatakuwa habari mbaya kwa uchumi.

"Tumeona kwamba hakuna mgogoro kati ya ukuaji mkubwa wa kiuchumi na ulinzi wa mazingira", Rais Obama amesema.

Ni mkutano kabambe unaowakusanya wajumbe 10 000, Marais na viongozi wa serikali 150i, maelfu ya waandishi wa habari na wataalamu.

Mkutano kuhusu hali ya hewa,  wito watolewa kwa kuiokoa dunia.
Mkutano kuhusu hali ya hewa, wito watolewa kwa kuiokoa dunia. LOIC VENANCE/UNTV/AFP

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.