Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHUNGUZI-UGAIDI-MAUAJI-USALAMA

Mashambulizi ya Paris: ndugu watatu wahusishwa katika uchunguzi

Ndugu watatu, ikiwa ni pamoja na mmoja wa watu waliojitoa mhanga wamehusika katika uchunguzi wa mashambulizi yaliotokea katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, vyanzo vilio karibu ya uchunguzi vimebaini Jumapili hii.

Ujumbe na maua vikiwekwa kwenye eneo la Jamhuri jijini Paris, Novemba 15, 2015, baada ya mashambulizi yaliosababisha vifo vya watu wengi.
Ujumbe na maua vikiwekwa kwenye eneo la Jamhuri jijini Paris, Novemba 15, 2015, baada ya mashambulizi yaliosababisha vifo vya watu wengi. PATRICK KOVARIK/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mmoja alikufa katika mashambulizi, wa pili yuko chini ya ulinzi nchini Ubelgiji, bila hata hivyo kujua kama alishiriki katika mashambulizi au la, na Idara zinaxopambanadhidi ya ugaidi hazina taarifa kuhusu mtu wa tatu. Mtu huyo wa tatu anaweza kuwa mmoja wa waliojitoa mhanga au kuwa mafichoni, vyanzo vilio karibu na uchunguzi vimeongeza. Ubelgiji imetoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwake.

Washambuliaji hao walikua wakiishi jijini Brussels, moja ya vyanzo hivyo imebaini, bila kujua uraia wao. Hata hivyo kwa mujibu wa moja ya vyanzo vilio karibu ya uchunguzi, washambuliaji hao ni raia wa Ufaransa, kwa mujibu wa chanzo kingine ni raia wa Ubelgiji.

Mmoja ametambuliwa kama mmoja wa waliojitoa mhanga. Wa pili amewekwa chini ya ulinzi nchini Ubelgiji. Chanzo cha polisi kitangaza kwamba mtuhumiwa huyo ameachiliwa, taarifa ambayo imekanushwa baadaye na Ofisi ya Mashtaka nchini Ubelgiji.

Vyeti vya mmoja wao - yule ambaye wachunguzi hawana taarifa yake - vimewasilishwa Jumamosi hii asubuhi wakati ukaguzi wa barabarani katika mpaka wa Ufaransa na Ubelgiji.

Wakaguzi wanajaribu kujua kama ni mhusika halisi ambaye aliyewasilishwa kwao au ni mmoja wa ndugu zake, ambaye alikamatwa mjini Brussels.

Mpaka hatua hii, wawili kati ya watu saba waliojitoa mhanga na kusababisha vilio katika mji wa Paris wametambuliwa, ikiwa ni pamoja na Omar Ismail Mostefai, Mfaransa , mwenye umri wa miaka 29.

Mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya watu 132 na kuwajeruhi wengine 350. Kundi la Islamic State limekiri kuhusika katika mauaji hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.