Pata taarifa kuu
UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Wabunge wa Ugiriki waitishwa kupiga kura juu ya mkataba

Makubaliano yaliyofikiwa Jumanne wiki hii kati ya Ugiriki na wakopeshaji wake yamewasilishwa Alhamisi Agosti 13 Bungeni. Wabunge wa Ugiriki wanatarajiwa kupiga kura juu mpango mgumu wa mabadiliko kwa miaka mitatu ijayo kwa ajili ya kupatiwa mpango mpya wa msaada wa kimataifa.

Waziri Mkuu Alexis Tsipras (kulia) anapaswa kulishawishi Bunge la Ugiriki ili lipigie kupiga kura Alhamisi jioni, muongozo wa nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Waziri Mkuu Alexis Tsipras (kulia) anapaswa kulishawishi Bunge la Ugiriki ili lipigie kupiga kura Alhamisi jioni, muongozo wa nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo. REUTERS/Alkis Konstantinidis
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na matakwa ya Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras, nakala yenye kurasa 400 ya makubaliano na wakopeshaji wa nchi hiyo inapaswa kujadiliwa katika kamati za bunge leo Alhamisi, na katika kikao, kabla ya kupiga kura, pengine usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa wiki hii.

Licha ya tawi la mrengo wa kushoto la Syriza kujiengua, chama cha Alexis Tsipras kina matumaini kuona makubaliano haya yanapitishwa kwa sauti 106 kutoka vyama vikuu vya upinzani. Hivyo makubaliano hayo yanaweza kuonekana kuwa na nguvu katika mkutano wa mawaziri wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro, uliopangwa kufanyika siku ya Ijumaa wiki hii.

Hata hivyo, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alielezea msimamo wa Ujerumani kwa ajili ya kuipatishia Ugiriki mkopo ili iweze kuilipa Euro bilioni 3,4 Benki kuu ya Ulaya Agosti 20, kabla ya saini ya mwisho ya mkataba huo. Hoja hiyo imetolewa pia na Finland.

Alexis Tsipras hataki kusikia kwa njia hiyo na ametoa matamshi makali kwa wale ambao, anaamini kuwa wana mpango wa siri wa kuanzisha upya kundi la nchi zinazozotumia sarafu ya Euro, wakitumia Ugiriki kama kisingizio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.