Pata taarifa kuu

EU yatoa Euro bilioni 2.4 kwa nchi zinazowapokea wahamiaji

Tume ya Ulaya imetangaza Jumatatu wiki hii kutoa Euro bilioni 2.4 kwa nchi zinazowapokea wahamiaji. Msaada huu kwa nchi wanachama 19 umepangwa kwa kipindi cha mwaka 2014 hadi 2020.

Wahamiaji walionusurika katika ajali ya kuzama kwa meli waliokuwemo wakiwasili katika mji wa Palermo, Sicily, wakiwa katika meli ya kijeshi ya Ireland Niamh, Agosti 6 mwaka 2015.
Wahamiaji walionusurika katika ajali ya kuzama kwa meli waliokuwemo wakiwasili katika mji wa Palermo, Sicily, wakiwa katika meli ya kijeshi ya Ireland Niamh, Agosti 6 mwaka 2015. REUTERS/Guglielmo Mangiapane
Matangazo ya kibiashara

Kama tangazo hili sio majibu ya moja kwa moja kwa ombi la msaada lililotolewa wiki iliyopita na Ugiriki pamoja na Italia, ni hatua ya kuzisaidia nchi zinazokabiliana na ongezeka kubwa la watu wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi.

Kwa tangazo hili, Tume ya Ulaya imehalalisha mipango 23 ya kitaifa katika suala la usimamizi wa ongezeko la uhamiaji. Fedha hizi, ziliyopangwa kwa kipindi cha mwaka 2014 hadi 2020, zitasaidia nchi nyingi zilioathirika na ongezeko la watu wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi. Italia itapewa Euro milioni 560, na Ugiriki itapewaEuro milioni 473. Lakini nchi nyingine wanachama ambazo zinakabiliwa na hali hii pia na tatizo hili pia zitanufaika na fedha hizo za Ulaya. Uhispania, Sweden au Bulgaria ni miongoni mwa nchi hizo.

Zoezi la kutolewa kwa fedha hizo na Tume ya Ulaya lilianza Machi na linatarajiwa kuendelea katika majuma yajayo. Njia hizi, zilizotokana na taratibu mbili za Ulaya, zina malengo tofauti. Lengo la wanza unakuja kusaidia nchi wanachama ili kuboresha uwezo wao wa mapokezi na ushirikiano kwa watu wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi. Lengo la pili linatilia mkazo umakini juu ya masuala ya usalama, ikiwa ni pamoja na kuboresha usimamizi na ufuatiliaji wa mipaka. Lakini fedha hizi pia zitasaidia kupambana dhidi ya ugaidi na aina zote za usalama barabarani.

Kwa tangazo hili, Tume ya Ulaya imsema inataka kuendesha kazi hii kwa moyo wa mshikamano. Moja ya njia ya kuzikumbusha nchi wanachama kuzingatia majukumu yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.