Pata taarifa kuu
UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Ugiriki yaepuka makampuni yake kufilisika

Baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo, Ugiriki na wakopeshaji wake wa kimataifa wamehitimisha Jumanne wiki hii mkataba kuhusu mpango wa tatu wa msaada wa Euro bilioni 85. Athens imeepuka kufilisika, lakini itachukua hatua ngumu za kiuchumi.

Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras (mgongo) na waziri wake mpya wa fedha Euclid Tsakalotos, Julai 6, katika mji wa Athens.
Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras (mgongo) na waziri wake mpya wa fedha Euclid Tsakalotos, Julai 6, katika mji wa Athens. REUTERS/Alkis Konstantinidis
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na mkutano huo, Athens hivyo imeepuka kushindwa kulipa na kwa sasa itaweza kulipa madani yake pamoja na malimbikizo. Mpango huu wa tatu msaada pia unaeleza mfumo wa bajeti ya ugiriki hadi mwaka 2018.

Hata hivyo, wakopeshaji wake, yaani Umoja wa Ulaya (EU), Benki Kuu ya Ulaya (ECB), Shirika la Fedha Duniani (IMF) na taasisi ya Ulaya inayokabiliana na mdororo wa uchumi (ESM), wamefanya makubaliano makubwa. Wametia mbele hususan umuhimu mdororo wa uchumi unaoikabili Ugiriki, ambayo imeendelea kudidimia tangu mwishoni mwa mwezi Juni na udhibiti wa mitaji, uliowekwa katika nafasi ya kuzuia benki kutokua na hofu ya kufilisika.

Hatua 35 zapewa kipaumbele

Hata kama wakopeshaji wake walikuwa wenye uelewa zaidi, Athens haijaachana na sheria zake kaliukali. Wakopeshaji wake wa kimataifa wamedai mkopo huo wa Euro bilioni 85 uendane na orodha ndefu ya marekebisho ya bajeti na mageuzi ya kimuundo kwa upande wa Athens. SKitabu kidogo chenye hatua 35 zilizopewa kipaumbele zitapitishwa wiki hii, wakati hatua nyingine zitapigiwa kura mwezi Oktoba.

Hatua hizi zilizopewa kipaumbele zinahusu mwisho wa likizo za kodi kwa wakulima, kupunguka kwa bei ya madawa hafifu, tathmini kamili ya mfumo wa hifadhi ya jamii ili kupata akiba ya kila mwaka ya mzunguko wa 0.5% ya pato la Taifa, ufafanuzi wa mfumo wa VAT katika visiwa vya Ugiriki au kupunguza vikwazo vya soko la nishati na gesi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.