Pata taarifa kuu
UFARANSA-IRAN-DIPOMASIA

Iran: ziara ya Laurent Fabius yachunguzwa kwa makini na Elysée

Laurent Fabius atafanya ziara ya kikazi Tehran leo Jumatano. Hii ni ziara ya kwanza ya waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa nchini Iran tangu miaka 12 iliyopita.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, ni waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa wa kwanza kujielekeza Iran tangu mika 12 iliopita.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, ni waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa wa kwanza kujielekeza Iran tangu mika 12 iliopita. REUTERS/Heinz-Peter Bader
Matangazo ya kibiashara

" Mtihani mgumu " kwa mujibu wa rais François Hollande " wa nia ya Iran wa kuwa na jukumu la mpatanishi katika ukanda ", baada ya makubaliano kuhusu mpang wa nyuklia wa Iran yalioafikiwa Julai 14.

Ziara ya Laurent Fabius nchini Iran itaangaliwa kwa makini na Ufaransa , ambayo kupitia waziri wake wa mambo ya nje aliikosoa Iran wakati wa mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, ambapo Iran ilimchukulia kama adui katika mpango wake endelevu.

" Fabius ni Ufaransa ", amesema rais wa Ufaransa François Hollande ambaye anasubiri, kuanzia sasa kutathmini " mwenendo wa Iran kwa namna atakavyokaribishwa waziri wake wa mambo ya nje ".

Jukumu la Iran kwa amani katika Ukanda

Rais wa Ufaransa amesisitiza hasa kuhusu jukumu la Iran katika jitihada za kupatikana kwa amani katika Mashariki ya Kati.

Rais wa Iran Hassan Rouhani anatakiwa " kuonyesha hisia zake za kijitihada, kuonyesha kwamba nchi yake inaweza kusaidia kutatua migogoro mikubwa inayoathiri Ukanda huo ", amesema François Hollande akitoa mfano wa haja ya kutoa ufumbuzi wa haraka kwa suala la Lebanon, lakini pia Syria, Yemen na Bahrain.

Rais wa Ufaransa amethibitisha uimara wake wakati ambapo makampuni ya Ufaransa yanajaribu kurejesha mguu katika soko la Iran. " Hatufikirii kwamba kanuni zetu za kisiasa zinaweza kusababisha mgongano katika masuala ya kiuchumi na kibiashara ", amesema rais Hollande.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.