Pata taarifa kuu
UNSC-IRAN-NYUKLIA-USALAMA-DIPLOMASIA

Iran: Umoja wa Mataifa waidhinisha Mkataba wa Vienna

Jumatatu wiki hii Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa pamoja bila kupingwa azimio linalohalalisha mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran ulioafikiwa juma lililopita mjini Vienna.

Upigaji kura kwa ishara ya kuinua mikono katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuidhinisha makubaliano ya Iran.
Upigaji kura kwa ishara ya kuinua mikono katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuidhinisha makubaliano ya Iran. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Nakala hii inapania kuondoa hatua kwa hatua vikwazo viliyochukuliwa dhidi ya Iran kwa sharti kwamba Iran iheshimu ahadi zake. Lakini vikwazo vya silaha na teknolojia ya makombora vitaendelea kwa kipindi cha mika 5 na 8.

Mabalozi wa Marekani na Iran waliketi kwenye meza ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilipitisha maazimio saba yaliyoendelea kuiadhibu Iran tangu mwaka 2006.

Pamoja na nakala hii mpya, ambayo inataja kuiondelea vikwazo Iran hatua kwa hatua, huu ni ukurasa mpya unaofunguka kwa mahusiano ya kimataifa. Huu ni ushindi kwa masuala ya diplomasia, kwa mujibu wa Samantha Power, mwakilishi wa Marekani kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa.

Ujumbe wa Iran pia umekaribisha mkataba huo, ambao ni ishara ya maridhiano katika "mgogoro usiokuwa wa lazima " kulingana na maneno ya balozi wa Iran kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Lakini hali inayouzunguka mkataba huo inaonesha kuwa njia ya kuaminiana bado ni ndefu kwa mujibu wa François Delattre, Balozi wa Ufaransa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa: " Mazungumzo katika wiki chache zijazo yatakuwa muhimu. Tutaamini kupitia vitendo na ahadi za Iran kuwa mkataba huu umepata mafanikio ".

Umoja wa Mataifa sasa unaanza kushughulikia rasmi suala la Iran kwa miaka kumi ijayo, kama inavyotakiwa na mkataba wa Vienna. Lakini nchi zenye nguvu tayari zilitangaza kwamba zingelingependa kuona kipindi hicho kinapunguzwa kwa miaka mitano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.