Pata taarifa kuu
UTURUKI-SYRIA-IS-MAPIGANO-USALAMA

Mapigano kwenye mpaka wa Uturuki na Syria

Mwanajeshi wa Uturuki ameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kusini mwa Uturuki baada ya kufyatuliwa risasi ziliyorushwa kutoka jimbo moja la Syria linaloshikiliwa na kundi la Islamic State.

Msafara wa magari ya jeshi la Uturuki kwenye mpaka kati ya Uturuki na Syria, karibu na mji wa Kilis, Julai 30 mwaka 2012.
Msafara wa magari ya jeshi la Uturuki kwenye mpaka kati ya Uturuki na Syria, karibu na mji wa Kilis, Julai 30 mwaka 2012. REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Uturuki limejibu shambulio hilo kwa kuendesha mashambulizi ya angani dhidi ya ngome za wanajihadi. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, magari ya kijeshi na vifaru vimeingia katika ardhi ya Syria.

Katikati ya mchana Alhamisi wiki hii risasi na makombora vimerushwa kutoka eneo linaloshikiliwa na kundi la Islamic State nchini Syria na kuelekezwa nchini Uturuki. Risasi na makombora hayo vimekua vikiwalenga wanajeshi wa Uturuki. Afisa wa jeshi la Uturuki ameuawa na wanajeshi wengine wengi wamejeruhiwa.

Jeshi la Uturuki limejibu mara moja, huku likirusha mabomu mengi kwenye ngome za wanajihadi. mapigano hayo yametokea karibu na mji wa Kilis, kwenye mpaka wa Uturuki na Syria. Mpiganaji mmoja wa Islamic State ameuawa, jeshi la Uturuki limearifu katika tangazo lililorusha hewani kwenye mtandao wake wa intaneti.

Gazeti linalounga mkono serikali Yeni Safak limearifu kuwa magari ya kijeshi ya Uturuki yaliingia katika ardhi ya Syria. Vifaru na ndege aina ya F-16 zilitumwa kusaidizana na wanajeshi wengine katika mji huo wa Kilis, amebaini hata hivyo mwandishi wa RFI katika mji wa Istanbul, Jérôme Bastion. Mkutano wa dharura katika Ikulu ya rais katika mji wa Ankara umeitishwa.

Hili ni tukio kubwa zaidi kutokea tangu kundi la Islamic State kuchukua udhibiti wa maeneo makubwa ya nchnii Syria zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Urushianaji huo risasi unatokea siku tatu baada ya shambulio la Suruç, lililohusishwa kundi la Islamic State. Shambulio hilo liligharimu maisha ya watu 32 na mamia wengine kujeruhiwa. Tangu wakati huo, serikali ya Uturuki ilitangaza kuimarisha hatua za usalama kwenye eneo lenye urefu wa kilomita 900 linalogawa Uturuki na Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.