Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA

Wagombea katika Uchaguzi Mkuu nchini Ufaransa waendelea kunadi sera zao

Wagombea urais nchini Ufaransa Marine Le Pen na Emmanuel Macron, wanaopewa nafasi ya kufanya vizuri katka Uchaguzi wa urais siku ya Jumapili, wanatafuta kura katika jiji kuu la nchi hiyo, Paris.

François Fillon, Benoît Hamon, Marine Le Pen, Emmanuel Macron na Jean-Luc Mélenchon.
François Fillon, Benoît Hamon, Marine Le Pen, Emmanuel Macron na Jean-Luc Mélenchon. Montage © RFI / REUTERS/Christian Hartmann
Matangazo ya kibiashara

Baada ya miezi na wiki za kampeni, hatimaye zimesalia siku chache kwa raia wa Ufaransa kufanya uamuzi wa kuchamgua kiongozi wao.

Kura za maoni kwa wiki kadhaa sasa zimekuwa zikiwapa nafasi kubwa Le Pen na Macron kushinda uchaguzi huu, kutokana na ahadi ambazo wameendelea kutoa kwa wapiga kura.

Marine Le Pen, katika kampeni zake amekuwa akisema anataka kurejesha na kulinda tamaduni za Ufaransa na kupambana na itikadi za kigaidi, huku kukiwa na hofu huenda akawashawishi raia wa Ufaransa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Macron naye ambaye aliwahi kuwa Waziri katika serikali ya rais François Hollande naye amekuwa akiahidi kuimarisha uchumi na kuongeza ajira.

Hata hivyo, François Fillon na Jean-Luc Melenchon ni wagombea wengine ambao pia wanaangaliwa kwa karibu sana na wapiga kura na wachambuzi wa siasa nchini Ufaransa.

Umaarufu wa Fillon ulishuka miezi kadhaa iliyopita, baada ya kudaiwa kutoa malipo kwa mkewe kwa kazi ambayo hakuifanya wakati alipokuwa Seneta. Melenchon ambaye alikuwa hapewi nafasi kubwa, siku za mwisho mwisho amekuwa akionekana akiwavutia waru wnegi kuhuduria mikutano yake ya kisiasa. Kura za maoni zinaoenesha kuwa huenda akamaliza katika nafasi ya tatu.

Ikiwa hakutakuwa na mshindi siku ya Jumapili atakayepata idaidi kubwa ya kura, kutakuwa na mzunguko wa pili tareheb7 mwezi Mei.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.