Pata taarifa kuu
UFARANSA

Ufaransa: Manuel Valls atangaza kumuunga mkono mgombea Macron

Waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa, Manuel Valls ametangaza kumuunga mkono mgombea wa mrengo wa kati Emmanuel Macron katika mbio zake za kuwania kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa April 23 mwaka huu.

Waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa, Manuel Valls.
Waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa, Manuel Valls. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Manuel Valls kwenye taarifa yake, amesema kuwa atampigia kura Macron kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi huo.

Akiulizwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni ikiwa atampigia kura Macron, Valls alisema “Ndio, kwasababu naamini haupaswi kufanya maamuzi ya hatari kwa jamhuri. Kwahivyo nitampigia kura Macron ambaye anatabiriwa kuwa atamshinda Marine Le Pen kwenye durua ya pili ya uchaguzi huo.

Uungaji mkono huu wa Valls kwa mgombea Emmanuel Macron unakuwa chachu kwake. Valls alijiondoa kwenye chama tawala cha Kisocialist baada ya kushindwa kupata uungwaji mkono na kuunda chama chake.

Macron kwa upande wake haraka sana alimuandikia ujumbe Valls kumpongeza kwa uamuzi wake wa kumuunga mkono.

Mgombea wa urais nchini Ufaransa, Emmanuel Macron.
Mgombea wa urais nchini Ufaransa, Emmanuel Macron. Reuters

Uamuzi wa Valls kumuunga mkono Macron unaonekana kama chuki aliyokuwa nayo dhidi ya mgombea wa chama chake cha Socialist Benoit Hamon aliyemshinda kwenye mchujo wa chama.

Katika hatua nyingine Jumanne ya wiki hii mke wa mmoja wa wagombea urais kwenye kinyang’anyiro cha mwaka huu, Francois Fillon, hatimaye amefunguliwa rasmi mashtaka dhidi yake ya kupewa kazi hewa na mume wake.

Penelope Fillon, alitumia muda wake siku ya Jumanne karibu siku nzima akihojiwa na maofisa wa polisi kutokana na ushiriki wake kwenye kashfa inayomkabili mume wake ambaye licha ya kupoteza umaarufu lakini bado ameendelea kusisitiza kutojiondoa kwenye mbio hizo.

Mume wake Francois Fillon nae aliwekwa chini ya uchunguzi mapema mwezi huu, akituhumiwa kutumia mamilioni ya pesa kwa familia yake kwa kazi ambayo hawakuifanya

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.