Pata taarifa kuu
UFARANSA-MDAHALO-SIASA

Wagombwa wakuu 5 nchini Ufaransa wachuana

Mdahalo wa televisheni kati ya wagombe wakuu watano katika uchaguzi wa urais nchini Ufaransa ulifanyika Jumatatu usiku na ulidumu saa moja kwenye runinga ya TF1ikiwa zimesalia wiki tano tu kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais.

Wagombea wakuu watano katika uchaguzi wa urais katika mdahalo ulioandaliwa na TF1, Machi 20, 2017.
Wagombea wakuu watano katika uchaguzi wa urais katika mdahalo ulioandaliwa na TF1, Machi 20, 2017. REUTERS/Patrick Kovarik/
Matangazo ya kibiashara

Wagombe wakuu watano, François Fillon, Benoît Hamon, Jean-Luc Mélenchon, Marine Le Pen, Emmanuel Macron walipambana katika mdahalo uliodumu saa moja.

Hata hivyo François Fillon, Emmanuel Macron na Marine Le Pen walikosoa utayarishwaji wa mdahalo huo, na kusikitika kukosekana kwa wagombea wengine sita waliopitishwa na Baraza la Katiba (Jean Lassalle, Nicolas Dupont-Aignan, Nathalie Arthaud, François Asselineau, Philippe Poutou na Jacques Cheminade).

Baada ya kila mmoja kupewa nafasi ya kuzungumza, tofauti mbalimbali zilijitikeza katika maswala kama usalama na uhamiaji, na kisha kutohemea upande wowote katika dini na na Uislamu.

Maswala haya yalizua hali ya sintofahamu na kila mmoja kujaribu kutoa sera zake kuhusu maswala hayo.

Mgombea wa FN alengwa mara kadhaa

Emmanuel Macron, anayepewa nafasi kubwa pamoja na mgombea wa chama cha FN kwa kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi, alilengwa na maswali mbali mbalimbali, lakini alijaribu kuonyesha pointi ambazo anakubaliana na baadhi ya washindani wake, ikiwa ni pamoja na François Fillon. "Nadhani ni kwa ajili yangu," amesema mgombea wa En Marche! wakati mgombea wa chama cha PS alipomuuliza "ahadi ya wazi" kuhusu uhuru wake kwa wafadhili wake wengi wa kampeni. "Ungelihi vibaya kama siningelikuwepo," alisema kwa kutania, wakati ambapo Marine Le Pen alichukua suala hilo kwa "maslahi binafsi" akimuunga mkono waziri wa zamani wa uchumi.

Mgombea wa chama cha pia mara nyingi alilengwa, hasa wakati Benoît Hamon alipomtuhumu kuwa "anakurupuka kwa maswala mablimbali" au wakati ambapo Mélenchon alipomtuhumu "kuchochea mambo mabaya kwa kila kitu." "Nataka kusimamisha uhamiaji, ni wazi, na ninahakikisha kabisa nia yangu," amesema kiongozi wa chama cha National Front (FN).

Midahalo miwili inapangwa kufanyika kabla ya Aprili 23, mmoja kwenye BFMTV na CNews Aprili 4, mwengine kwenye France 2 Aprili 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.