Pata taarifa kuu
UFARANSA - UCHAGUZI

Wagombea 11 wa Urais nchini Ufaransa wachuana vikali

Siku 19 kabla ya uchaguzi wa rais nchini Ufaransa, wagombea 11 katika uchaguzi huo wamechuana vikali hapo jana jumanne jioni katika mdahalo wa moja kwa moja kwenye televisheni za BFMTV na CNews. mada zilizogubikwa mdahalo huo ni pamoja na ajira, Usalama na maswala ya kijamii na ambao ulidumu kwa takriban saa nne.

mdahali wa wagombea 10 katika uchaguzi wa rais mwaka  2017 nchini Ufaransa, Philippe Poutou alikataa kupiga picha na wengine
mdahali wa wagombea 10 katika uchaguzi wa rais mwaka 2017 nchini Ufaransa, Philippe Poutou alikataa kupiga picha na wengine RFI/Bruno Faure
Matangazo ya kibiashara

Aliepewa nafasi ya kunzumza kwa mara ya kwanza katika mdahalo huo ilikuwa ni Nicolas Dupont-Aignan ambae alianza kwa makombora dhidi ya mshindani mwenzie Francois Fillon kuhusu mambo yanayotikisa kampeni hizo za uchaguzi. Mgombea huyo alisikika akisema kwamba "Nimekuwa nikiwahudumia wafaransa, bila hata hivyo kujihudumia"

Kuhusu swala ambalo kila mmoja alitakiwa kujibu kwa wakati wake kujieleza yeye ni nani, wagombea Emmanuel Macron na Marine Le Pen wanaotabiriwa na wengi kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi wameendelea kujitetea kwamba wao ndio wagombea wa mabadiliko ya kweli na wenye miradi iliowazi isiokuwa na chenga wala longolongo.

Upande wake Francois Fillon amejinadi kuwa ndie mgombea ataeleta ahueni na kuirejesha fahari ya kitaifa na kushirikiana bega kwa bega na wananchi wa Ufaransa wanaotaka muelekeo na usalama.

Naye mgombea wa chama cha kisocialisti Benoît Hamon, amejinadi kuwa rais anaefahamu jukumu lake, muaminifu, mpambanaji na mwenye kujua utu.

Jean-Luc Mélenchon ambae ameendelea kusisitiza kuhusu swala la uchumi na kueleza utayari wake wa kuliongoza taifa

Hata hivyo mgombea Marine Le Pen ameonekana kushambuliwa na wagombea kama vile Emmanuel Macron, Benoit Hamon na Francois Fillon kuhusu mpango wake wa kuindoa Ufaransa kwenye Umoja wa Ulaya iwapo chama chake kitashinda uchaguzi mkuu wa rais.

Mgombea Philippe Poutou alizua mjadala hata kabla ya kuanza kwa mdahalo huo pale alipokataa kushirikiana na wagombea wengine katika upigaji picha ya pamoja.

Mdahalo huu uliopeperushwa moja kwa moja kupitia BMTV na Cnews uligubikiwa na mvutano mkubwa miongoni mwa wagombea ambao walishambuliana kuhusu

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.