Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MADURO-USALAMA-SIASA

Maandamano ya kumtaka Rais Maduro kuondoka madarakani yaendelea Venezuela

Mamia kwa maelfu ya raia wa Venezuela waliandamana nchini kote Jumatano, Oktoba 26 kwa kuitikia wito wa upinzani. Changamoto: kuweka shinikizo kwa Baraza la Kitaifa la Uchaguzi ili kuanzisha upya mchakato wa kura ya maoni.

Waandamanaji katika mji wa Caracas wakiandamana dhidi ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, Oktoba 26.
Waandamanaji katika mji wa Caracas wakiandamana dhidi ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, Oktoba 26. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins
Matangazo ya kibiashara

Kwa miezi kadhaa, muungano wa upinzani MUD, ulio na idadi kubwa ya wabunge nchini humo, umeendelea na harakati zake katika katika mchakato wa kura ya maoni dhidi ya Rais Nicolas Maduro. Hatua ya kwanza ilisahihishwa mapema mwezi Agosti; hatua ya pili ilikuwa inatazamiwa kuanza Jumatano wiki hii. Lakini wiki iliyopita Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi iliamua "kuchelewesha mchakato huo hadi itakapotangazwa siku nyingine", kwa kuzingatia maamuzi ya mahakama za mikoa kadhaa. Wakati ambapo kura dhidi Nicolas Maduro imeahirishwa mwaka huu, upinzani haukubali kushindwa hadi na hivyo kuandandaa Jumatano wiki hii maandamano makubwachini ya kauli mbiu: ". kuidhibiti nchi ya Venezuela"

Maandamano dhidi ya Rais wa Venezuela mwenye mrengo wa kijamaa Nicolas Maduro yamefanyika katika maeneo yote ya nchi hiyo, huku baadhi waandamanaji wakifanya vurugu.

Mashahidi wanasema vikosi vya usalama vimepambana na waandamanaji katika miji mbalimbali, huku watu kadhaa wakijeruhiwa na wengine kuwekwa kizuizini.
maandamano hayo ni ya wito wa kumtaka Rais Maduro ajiuzulu juu ya kushindwa kwake katika usimamizi wa Uchumi.

Muungano wa upinzani nchini humo umetoa masaa 12 ya maandamano ya pamoja siku ya ijumaa ili kuongeza shinikizo kwa Rais huyo kujiuzulu, ambapo wanamshutumu kwa ukiukwaji wa Demokrasia, na bunge la nchi hiyo linamshutumu kwa kutaka kupanga mapinduzi.

Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Venezuela amesema polisi mmoja alipoteza maisha wakati wa maandamano hayo. Waziri huyo amesema polisi aliyepoteza maisha alipigwa risasi na watu waliokua wakiandamana. amebaini pia kwamba polisi wengine wawili walijeruhiwa.

PoliMiranda, ambayo ni polisi ya jimbo la Miranda, ambapo Henrique Capriles, ni mkuu wa jimbo hilo, amethibitisha kifo cha ploisi huyo, lakini haijatoa maelezo kuhusu mazingira kifo chake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.