Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA

Venezuela: mkutano wa kisiasa kuhusu suala la kura ya maoni

Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi nchini Venezuela (CNE) inakutana Jumatatu hii ili kujibu upinzani unaotaka kuandaa kura ya maoni juu ya kujiuzulu kwa Rais Nicolas Maduro, wakati ambapo nchi hii yenye utajiri wa mafuta inakabiliwa na mgogoro wa kiuchumi.

Rais Nicolas Maduro Mei 16, 2016 Caracas.
Rais Nicolas Maduro Mei 16, 2016 Caracas. JUAN BARRETO/AFP
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi (CNE) ingelitoa uamuzi wake Jumanne wiki iliyopita lakini, siku hiyo, mamlaka hiyo, ambayo upinzani unaituhumu kuipendelea serikali, ilitangaza kwamba inaahirisha kikao chake hadi Agosti 1, ikisema haiwezi kushinikizwa na mtu yeyote.

Hata hivyo, haijathibitika kwamba Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi itatoa uwamuzi wake aukuweka wazi matokea ya mkutano huo.

Rais Nicolas Maduro alichaguliwa mwaka 2013 kwa kipindi cha miaka 7 hadi mwaka 2019, lakini anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kutoka kwa bunge lenye wajumbe wengi kutoka muungano wa vyama vya mrengo wa kati na wale wanaopinga nadharia ya aliyekua rais wa nchi hiyo Hugo Chavez wakiomba kura ya maoni dhidi Maduro kabla ya mwisho wa mwaka 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.