Pata taarifa kuu
VENEZUELA-COLOMBIA

Umati wa raia wa Venezuela waingia Colombia kutafuta chakula

Raia wa Venezuela wamevuka kwa wingi mpaka na Colombia, uliofungwa kwa karibu mwaka mmoja na kufunguliwa kwa muda Jumapili hii, kwenda kununua chakula na madawa, ambavyo ni haba katika nchi yao inayokumbwa na mgogoro.

Raia wa Venezuela wakivuka mpaka na kuingia Colombia kukunua chakula.
Raia wa Venezuela wakivuka mpaka na kuingia Colombia kukunua chakula. REUTERS/Carlos Eduardo Ramirez
Matangazo ya kibiashara

"Tuna furaha kwa sababu tuna chakula. Nchini Venezuela, hakuna chochote! Hata dawa kwa za watoto hamna! Viongozi wahodhi chakula. Kile anachosema rais, kwamba kuna chakula, ni uongo! " Tulia Somaz amesema akiliambia shirika la habari la AFP, huku akipongezwa na wenzake ambao wamekua wakivamia maduka makubwa ya mji Cucuta, mji wa Colombia ulio kwenye mpaka na mji wa San Antonio katika jimbo la Tachira.

"Hatuna hata sabuni ya kufua nguo," amesikitika mwanamke mmoja makamo, ambaye kama maelfu ya rara wengine wa Venezuela wamekua wakivuka kwa mgu mita 700 zinazoachanisha miji hiyo miwili.

Baada ya kuagiza kufungwa kwa mpaka mwezi Agosti mwaka jana kutokana na sababu za usalama, Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, ameruhusu watu kuvuka kwa mgu madaraja ya Simon Bolivar (Venezuela) na Francisco de Paula Santander (Colombia).

Alfajiri, foleni ndefu zilionekana mbele ya ofisi za mpakani za Venezuela wakisubiri kufunguliwa kwa mpaka. Wengi walilala usiku ndani ya magari yao ili waweze kufika mpaka mapema asubuhi. Serikali ya Venezuela imetangaza kwamba mpaka utakua wazi kwa kipindi kisichozidi masaa 12.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.