Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA

Kura ya maoni dhidi ya Maduro haitofanyika mwaka 2016

Viongozi wa Tume ya Uchaguzi nchini Venezuela wametangaza Jumatano kuwa kura ya maoni dhidi ya Nicolas Maduro itafanyika baada ya mwezi Januari 2017 na hivyo kukatisha matumaini ya upinzani waliokua wanataka rais aondoke madarakani.

Rais wa Venezuela Nicolás Maduro, akosolewa na wapinzani wake kuwa ameshindwa kuinua uchumi wa nchi yake..
Rais wa Venezuela Nicolás Maduro, akosolewa na wapinzani wake kuwa ameshindwa kuinua uchumi wa nchi yake.. DR/Reuters/Palacio de Miraflores
Matangazo ya kibiashara

Kwa maana hiyo ili uchaguzi wa mapema ufanyike, kura ya maoni inapaswa kufanyika ifikapo Januari 10, 2017 na kuwa na mafanikio, lakini kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kura ya maoni "inaweza kufanyika katikati ya mwezi Februari 2017".

Hayo yakijiri mamia ya madereva wa mabasi katika mji wa Caracas wamefanya mgomo na kuamua kusimamisha kazi Jumatano wiki hii wakidai kuongezwa kwa nauli na kurahisishiwa kupata vipuri kwa ajili ya magari yao. Mgomo huo umezorotesha sgughuli nyingi katika mji mkuu wa Venezuela.

Madereva wa mabasi walizuia kwa muda wa masaa tisa moja ya barabara kuu ya mji wa Caracas, Venezuela.
Madereva wa mabasi walizuia kwa muda wa masaa tisa moja ya barabara kuu ya mji wa Caracas, Venezuela. (AFP/JUAN BARRETO)

Baada ya kuandamana na magari yao upande wa mashariki wa mji huo wenye wakazi milioni mbili, aliamua kuegesha magari yao mbele ya Wizara ya Uchukuzi, na hivyo kuzuia kwa muda wa masaa tisa moja ya barabara kuu ya mji.

"Kama hatupati majibu, tutaendelea na mgomo wetu," amesema Hugo Ocando, msemaji wa madereva wa mabasi, baada ya kusitisha mgomo huo, uamuzi uliyochukuliwa baada ya kupata ahadi ya kupokelewa na Waziri wa Uchukuzi Ricardo Molina.

Kwa mujibu wa Ocando, takriban madereva 25,000 wanaunga mkono mgomo huo wakidai kuongezwa kwa bei ya nauli kutoka Bolivars (sarafu ya Venezuela) 45 hadi 60, sarafu hiyo imepoteza thamani ya senti 10 ikilinganishwa na Dola.

Maandamano yanaweza kuenea katika miji mingine nchini Venezuela kama Bw Molina hatozingatia madai yao "kwa sababu ni tatizo ambalo linaathiri nchi nzima," Erick Zuleta, kiongozi wa Shirikisho la kitaifa la Magari ya Usafiri (FNT), ameambia vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.