Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MERCOSUR

Venezuela yalaani uamuzi wa Mercosur

Hali ya mvutano imeendelea kujitokeza kati ya Jumuiya ya nchi za Amerika ya Kusini (Mercosur) na Venezuela. Jumuiya hii imeamua kuinyang'anya Venezuela uenyekiti ambapo kila mwaka nchi nne zinazounda jumuiya hiyo zimekua zikipokezana uenyekiti. Hata hovyo serikali ya Venezuela imefutilia mbali uamuzi huo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, Delcy Rodriguez,Septemba 2, mjini Caracas.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, Delcy Rodriguez,Septemba 2, mjini Caracas. REUTERS/Marco Bello
Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa haijajulikana nchi inayoshikilia uenyekiti wa jumuiya ya nchi za Amerika ya Kusini (Mercosur). Serikali ya Venezuela inadai kuwa bado inashikilia uenyekiti wa jumuiya hiyo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela amekataa kutambua uamuzi wa nchi nne wanzilishi wa Mercosur, ambayo ni "kinyume na mikataba ya jumuiya hiyo," Delcy Rodríguez ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Jumanne hii Septemba 13, Argentina, Brazil, Paraguay na Uruguay wamekubaliana kwa pamoja kushikilia uenyekiti wa Mercosur. Wanaishutumu Venezuela kutokuheshimu "vifungu vya sheria" vya jumuiya ya nchi za Amerika ya Kusini.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil , José Serra, Venezuela siyo nchi ya kidemokrasia. Inaonekana kutoheshimu utaratibu huo. Uruguay, ambayo ilijizuia wakati wa kupiga kura - imeamua kuitaja Venezuela kama nchi ya 'demokrasia ya kimabavu".

Licha ya tofauti zao, Jumuiya ya nchi za Amerika ya Kusini (Mercosur) imetoa kauli ya mwisho kwa serikali ya Venezuela: kama itakua bado haijazingatia sheria katika masuala ya uchumi hadi Desemba 1, nchi hiyo itaondolea kuwa mwanachama wa jumuiya ya nchi za Amerika ya Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.