Pata taarifa kuu

Venezuela: upinzani na wafuasi wa serikali kundamana Caracas

Nchini Venezuela, wapinzani na wafuasi wa utawala uliopo madarakani wameandamana Alhamisi hii Septemba 1 katika mitaa mbalimbali ya mji mkuu wa nchi hiyo, Caracas. Venezuela inaendelea kuathirika na mgogoro wa kisiasa na kiuchumi.

Maandamano katika mitaa ya mji mkuu wa Venezuela, Caracas.
Maandamano katika mitaa ya mji mkuu wa Venezuela, Caracas. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins
Matangazo ya kibiashara

Hali hii inajiri wakati ambapo baadhi ya viongozi wa upinzani wamekamatwa na serikali ya Nicolas Maduro. Upinzani bado unaendelea kudai kura ya maoni juu ya kumuondoa mamlakani Rais wa sasa NIcolas Maduro.

Maandamano makubwa yamefanyika Alhamisi hii Septemba 1 nchini Venezuela katika hali ya wasiwasi. Wapinzani dhidi ya serikali ya Nicolas Maduro wametakiwa kushiriki katika mkutano wa hadhara kudai kufanyika kwa kura ya maoni dhidi ya rais madarakani. Wafuasi wa Rais Nicola Maduro pia wamemiminika mitaani siku hii ya Alhamisi katika mji mkuu, Caracas, ili kumuunga mkono rais wao.

"Raia wote wa Venezuela wanajianda kwa haki ya kupiga kupiga kura," awali ulisema muungano wa upinzani wa MUD, ambao ulitoa wito kwa wananchi wa Venezuela "kuudhibiti mji wa Caracas." Pamoja na maandamano hayo, upinzani ulitaka kuishinikiza serikali kuandaa kwa haraka kura ya maoni dhidi ya Rais Nicolas Maduro.

Wakati huo huo, rais aliwataka wafuasi wake "kuushikilia mji wa Venezuela", kwa minajili ya "kutetea mapinduzi " yaliyoanzishwa na mtangulizi wake, Hugo Chavez, aliyekaa madarakani kati ya mwaka 1999 hadi 2013. Nicolas Maduro pia ameutishia upinzani. Kitendo chochote cha vurugu kitadhibiwa na kifungo, ameonya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.