Pata taarifa kuu
VENEZUELA-NICOLAS MADURO

Serikali ya Venezuela na upinzani kukutana kwa mazungumzo Jumapili

Serijkali ya Kisoshalisti ya Venezuela na upinzani watakutana kwenye meza ya mazungumzo Jumapili mwishoni mwa wiki hii, wakati ambapo nchi hii inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa na maandamano yanayoendelea tangu kusimamishwa kwa mchakato wa kura ya maoni ilio kuwa ikimlenga Rais Nicolas Maduro.

Makundi ya vijana yalichoma moto takataka na kuweka vizuizi kwenye barabara za mji wa San Cristobal, nchini Venezuela.
Makundi ya vijana yalichoma moto takataka na kuweka vizuizi kwenye barabara za mji wa San Cristobal, nchini Venezuela. Reuters / Carlos Eduardo Ramirez
Matangazo ya kibiashara

Pande zote mbili zitakutana katika kisiwa cha Margarita, serikali, upinzani na mwakilishi wa Papa Francis (balozi) wa Vatican nchini Venezuela, wametangaza Jumatatu hii.

"Mazungumzo yamepangwa kufanyika," Jorge Rodriguez, mmoja wa viongozi wa chama cha Kisoshalisti madarakani, ameviambia vyombo vya habari. Mazungumzo yatafanyika chini ya usimamizi wa Vatican, UNASUR (Umoja wa Mataifa ya Amerika Kusini) na marais watatu wa zamani nchi hiyo.

Mazungumzo ya awali kati ya kambi hizi mbili hayakuza matunda yoyote.

Nicolas Maduro, ambaye yupo katika ziara ya nchi zinazozalisha mafuta alipokelewa kwa mazungumzo na Papa Francis mjini Vatican. Kiongozi huyu wa Kanisa Katoliki alimtaka Rais Nicolas MAduro kuanzisha mazungumzo na upinzani.

"Hatimaye, tunaanzisha mazungumzo kati ya upinzani na serikali halali," Maduro amesema mjini Roma, baada ya kupokelewa na Papa Francis.

Papa Francis amemuomba Bw Maduro "kuendelea na njia ya mazungumzo ya dhati na yenye kujenga ili kupunguza mateso ya wananchi wa Venezuela, na jhasa watu maskini, na hivyo kunjenga hali ya mshikamano wa kijamii ambapo itawapelekea wananchi kuwa na matumaini ya mustakabali wa nchi yao, "Papa Francis amesema katika taarifa yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.