Pata taarifa kuu
BRAZIL-SIASA-RUSHWA

Brazil: Mahakama Kuu yafutilia mbali madai ya Rousseff

Mahakama Kuu ya Brazil, Alhamisi hii usiku, imejadili madai matatu ya utaratibu wa kujiuzulu yanayomlenga Rais Dilma Rousseff, ikiwa zimesalia siku mbili ya kura muhimu ya Wabunge juu kubakia kwake madarakani au la.

Rais wa Brazil Dilma Rousseff, Machi 22, 2016 Brasilia.
Rais wa Brazil Dilma Rousseff, Machi 22, 2016 Brasilia. REUTERS/Adriano Machado
Matangazo ya kibiashara

Majaji wa mahakama ya juu walichukua uamuzi Alhamisi usiku ili kukamilisha kazi yao kabla ya ufunguzi wa mkutano wa Wabunge Ijumaa hii asubuhi, mkutano ambao umepangwa kuchukua siku tatu, hadi Jumapili.

Mahakama Kuu imefutilia mbali jaribio la bahati ya mwisho ya Rais Rousseff la kuiomba Mahakama hiyo kuzuia utaratibu wa kujiuzulu ulioanzishwa dhidi yake.

Alhamisi mchana, Rais Dilma Rousseff aliwasilisha mashataka yake mbele ya Mahakama ya juu ili kuiomba ifute utaratibu huo baada ya kuona kuwa anaendelea kutishwa na hali hiyo kila kukicha.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, José Eduardo Cardozo, ambaye aliwasilisha mashataka hayo alishutumu utaratibu huo, akisema kuwa "unakiuka kanuni za kesi na haki kwa upande wa utetezi."

Rais kutoka chama cha mrengo wa kushoto anatuhumiwa na upinzani kutumia kwa maksudi fedha za umma katika uchaguzi wake wa mwaka 2014 na mwanzoni mwa mwaka 2015 bila kujali ukubwa wa Mapungufu na kushuka kwa uchumi.

Dilma Rousseff anakanusha kuwa "madai" ya bajeti yanayotumiwa na watangulizi wake ni "uhalifu wa kimadaraka" ambao unaweza kusababisha kutimuliwa mamlakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.