Pata taarifa kuu

AFCON 2024: Kocha wa Côte d’Ivoire Jean-Louis Gasset afutwa kazi

Kocha wa Côte d'Ivoire, raia wa Ufaransa, Jean-Louis Gasset, amefutwa kazi Jumatano hii, Januari 24, siku mbili baada ya timu yake kufedheheshwa dhidi ya Equatorial Guinea. Nafasi yake inachukuliwa na mchezaji wa zamani Emerse Fae.

Kocha mkongwe Jean-Louis Gasset wa Côte d'Ivoire afukuzwa kazi siku mbili baada ya timu yake kufungwa na Guinea Equatorial 4-0.
Kocha mkongwe Jean-Louis Gasset wa Côte d'Ivoire afukuzwa kazi siku mbili baada ya timu yake kufungwa na Guinea Equatorial 4-0. REUTERS - LUC GNAGO
Matangazo ya kibiashara

 

Uvumi kuhusiana na kutimuliwa kwa kocha wa Côte d'Ivoire ulichochea soka ya nchi hiyo tangu Tembo wa Côte d'Ivoire kushindwa dhidi ya Equatorial Guinea (4-0), taarifa hii imethibitishwa kwa RFI wakati wa mchana na afisa katika uongozi wa timu ya taifa ya Côte d’Ivoire kabla ya taarifa kutoka Shirikisho la Soka la Côte d’Ivoire haijaweka mambo bayana. Jean-Louis Gasset hafai tena kuwasimamia Tembo wa Côte d’Ivoire. Matokeo ya moja kwa moja ya AFCON walioshindwa kwa michezo miwili, kushindwa mfululizo na timu inayojitahidi.

Akikosolewa kwa uchaguzi wake wa kiufundi na ugumu wa timu yake, Jean-Louis Gasset, hatimaye na naibu wake Ghislain Printant wamefukuzwa kazi, "kwa matokeo yasiyotosha, kwa mujibu wa mkataba wenye lengo unaowaunganisha na FIF", Shirikisho la Soka la Côte d’Ivoire limetangaza.

Hata kama matumaini ya kufuzu kwa hatua ya 16 bado yamesalia kabla ya mechi za mwisho za hatua ya makundi, viongozi wa Côte d’Ivoire hawakutaka kusubiri, kutokana na shinikizo la watu wengi.

  

Makabiliano yalizuka uwanjani mwishoni mwa mechi, ambayo yalizuiliwa haraka. Baada ya mechi hiyo, baadhi ya wafuasi waliokuwa wenye hasira waliharibu mabasi kwenye barabara inayotoka uwanja wa Ebimpé kuelekea mji wa Abidjan, kabla ya utulivu kurejea baada ya polisi kutumia vitoa machozi.

Sasa ni mchezaji wa zamani wa kimataifa Emerse Fae (mechi 44) ambaye anachukua hatamu ya kuinoa Côte d’Ivoire kwa changamoto kubwa labda, ikiwa Côte d'Ivoire itafuzu, pambano dhidi ya bingwa mtetezi, Senegal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.