Pata taarifa kuu

CAN 2024: DRC yailazimu Morocco kutoka sare ya kufungana 1-1

Morocco na DRC zimetoka sare ya kufungana (1-1), siku ya Jumapili, Januari 21 kwenye uwanja wa Laurent Pokou mjini San Pedro. Ikiwa Simba ya Atlas ilitangulia kufunga kwa haraka sana kupitia mchezaji Achraf Hakimi, DRC ilirejea uwanjani mwishoni mwa kipindi cha pili na kufunga bao la kusawazisha kupitia mchezaji Silas Katompa Mvumpa.

Mmorocco Azzedine Ounahi na Mkongo Silas Katompa Mvumpa wakati wa mechi kati ya Morocco na DRC mjini San Pedro, Januari 21, 2024.
Mmorocco Azzedine Ounahi na Mkongo Silas Katompa Mvumpa wakati wa mechi kati ya Morocco na DRC mjini San Pedro, Januari 21, 2024. © AFP / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

 

Kutoka kwa mwandishi wetu maalum huko San Pedro,

Tofauti na mechi iliopita dhidi ya Tanzania, Morocco haikulazimika kusubiri muda mrefu sana kuona lango la DRC. Mchezaji Achraf Hakimi, amepata ya fursa ya kuona bao la DRC kupitia kona iliyopigwa na Hakim Ziyechkatika dakika ya 6. Mchezaji huyo wa zamani wa Madrid amefunga bao lake la kwanza kwenye mechi hiyo, akiwa ndiye aliyepiga pasi za mwisho dhidi ya Tanzania. Hapo awali, Youssef En-Nesyri alimlazimisha kipa wa Kongo kuokoa mpira maeingira tatanishi, baada ya mpira wa kichwa uliopigwa na mchezaji huyo wa Sevilla FC katika dakika ya pili.

Fiston Mayele, mchezaji wa DRC akikabiliana na mchezaji wa Morocco Achraf Hakimi wakati wa mechi kati ya Morocco na DRC mjini San Pedro, Januari 21, 2024.
Fiston Mayele, mchezaji wa DRC akikabiliana na mchezaji wa Morocco Achraf Hakimi wakati wa mechi kati ya Morocco na DRC mjini San Pedro, Januari 21, 2024. © AFP / SIA KAMBOU

Ikiwa DRC walipata nafasi nyingi nzuri dhidi ya Zambia katika mechi waliocheza hivi karibuni, imekuwa tofauti dhidi ya Simba ya Atlas. Ilibidi kusubiri hadi dakika ya 33 kuona Leopards wakikosa nafasi nzuri: kona iliyopigwa na Kakuta ilipanguliwa na Selim Amallah na kuelekea kwa Chancel Mbemba, aliyekuwa tayari kuuweka tu wavuni, lakini aliwashangaza wengi kwa kushindwa kusukuma mpira huyo wavuni.

DRC wangelifunga bao lao la kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti iliyopatikana baada ya Selim Amallah kunawa mpira katika eneo la hatari. Lakini Cédric Bakambu alishindwa kulionalango la Yassine Bounou baada ya mpira kugonga mwamba wa kushoto katika dakika ya 41.

Mabadiliko yaokoa DRC

Bao la kusawazisha hatimaye limepigwa katika dakika ya 77 na umati wa mashabiki ukapaza sauti katika uwanja wa Laurent Pokou. Elia Meschack akimpigia krosi Silas Katompa Mvumpa, mchezaji aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi, ambaye hakusita kuliona lango la Yassine Bounou. Baada ya bao hilo la kusawazisha, DRC imeshindwa kufunga bao la pili baada ya krosi ya Elia Meschack kwa Samuel Mououssamy alijijuta amepoteza mpira katika dakika ya 79.

Mmorocco Achraf Hakimi na Mkongo Silas Katompa Mvumpa, wote wawili waliofunga mabao wakati wa mechi kati ya Morocco na DRC mjini San Pedro, Januari 21, 2024.
Mmorocco Achraf Hakimi na Mkongo Silas Katompa Mvumpa, wote wawili waliofunga mabao wakati wa mechi kati ya Morocco na DRC mjini San Pedro, Januari 21, 2024. © AFP / SIA KAMBOU

Morocco, ambayo ilitaka kufuzu kwa hatua ya 16 bora siku ya pili, itasubiri. Sébastien Desabre, kocha wa Leopards, hakuwa ameficha nia yake ya kupata angalau sare dhidi ya timu imendelea kupewa nafasi kubwa ya kushinda kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) la mwaka huu. Wakati huo huo, Morocco, iliyopigwa na Ufaransa katika nusu fainali ya Kombe la Dunia lililopita mnamo Desemba 2022 huko Qatar, ilishinda mara moja Kombe la AFCON, mnamo mwaka wa 1976 nchini Ethiopia.

Nchini Côte d'Ivoire, hili sasa ndilo taji ambalo vijana wa Walid Regragui wanalenga, na si kingine. Wakati wa toleo la mwisho la 2022 nchini Cameroon, Atlas Lions walitolewa katika robo fainali na Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.