Pata taarifa kuu
AFCON 2023

Chris Hughton aonesha ghadhabu baada ya sare ya dhidi ya Misri

San Pedro, Cote d'Ivoire – Kocha Mkuu wa Black Stars ya Ghana, Chris Hughton ameelezea masikitiko yake kufuatia sare ya 2-2 dhidi ya Misri katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2023 uwanjani Felix Houphouet Boigny jijini Abidjan nchini Ivory Coast.

Kocha wa Ghana, Chris Hughton kwenye mechi dhidi ya Misri mnamo 18/01/2024 uwanjani Felix Houphouet Boigny jijini Abidjan
Kocha wa Ghana, Chris Hughton kwenye mechi dhidi ya Misri mnamo 18/01/2024 uwanjani Felix Houphouet Boigny jijini Abidjan © CAF
Matangazo ya kibiashara

Rui Vitoria wa Misri kwa upande mwingine, alifurahishwa na dhamira ya wachezaji wake baada ya Mafarao hao kutoka nyuma mara mbili n kudumisha mwanzo mzuri wa kutopoteza mechi yoyote.

Ghana iliongoza mara mbili na kuiruhusu Misri kupata alama moja kwenye mchezo huo.

Licha ya matokeo ya kukatisha tamaa, Chris Hughton hajakata tamaa.

Tutaendelea kupambana. Ni kweli kwa sasa kuna hali ya kuchanganyikiwa kwenye chumba chetu cha kubadilishia nguo. Timu yetu ilistahili zaidi ushindi, lakini mpira wa miguu uko hivyo. Inakatisha tamaa. Makosa mawili yalitugharimu mechi.

Wachezaji wa Ghana wakisherehekea bao la Mohammed Kudus
Wachezaji wa Ghana wakisherehekea bao la Mohammed Kudus © CAF

Bao la kwanza la Misri lilipatikana dakika ya 69 wakati Omar Marmoush, tishio katika mechi yote, aligubikia pasi mbaya ya Iñaki Williams kisha kumchenga mlind lango Richard Ofori na kufunga bao, kabla ya nguvu mpya Osmane Bukari kunyang'anywa mpira na Trezeguet katika eneo lake na kutengeneza bao la kusawazisha la Mostafa Mohamed.

Bukari alitolewa baadaye dakika ya 89 na nafasi yake kuchukuliwa na Joseph Paintsil. Kocha Houghton akielezea uamuzi wake.

Kwanza, ningependa kusema kwamba tunampenda Osmane. Ilibidi nimtoe kwa sababu makosa yake yalikuwa yameanza kuathiri utendaji wake.

Huku macho yote yakielekezwa kwa mechi inyofuata dhidi ya Msumbiji, kocha mkuu wa Black Stars alisema, “Hakuna tena timu ndogo barani Afrika. Tunajua ni mechi ambayo lazima tushindeTunajiandaa kwa mechi ngumu dhidi yao. Mahesabu tayari yameshafanyika, tunahitaji ushindi ili kutekeleza ndoto yetu na najua tunaiweza.”

Kiungo wa Ghana, Mohammed Kudus ambaye aitajwa mchezaji bora wa mechi kufuatia kufunga magoli yote mawili ya Ghana alisisitiza haja ya kulenga mechi ijayo huku akiwahongera wachezaji wote wa Ghana kwa kujituma zaidi.

Kwa upande mwingine kocha wa Misri, Rui Vitoria alifurahishwa na dhamira na utendakazi wa wachezaji wake, walipotoka nyuma mara mbili na kudumisha mwanzo wao mzuri mashindanoni wa kutopigwa mechi yoyote.

Nina imani kubwa na timu yangu. Niliona wanaume usiku huu ambao walipigana hadi mwisho, ushindi pekee ndio uliotukwepa. Tulionyesha sifa nzuri jioni hii dhidi ya Ghana ambayo imeamka. Wachezaji walitekeleza maagizo yetu kikamilifu.

Kocha wa Misri, Rui Vitoria kwenye kikao na wanahabari
Kocha wa Misri, Rui Vitoria kwenye kikao na wanahabari © CAF

Mreno huyo hata hivyo hakuthibitisha hali na kiwango cha jeraha la mshambuliaji Mohamed Salah ambaye alilazimika kutolewa dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza kutamatika.

Kwa sasa, siwezi kuzungumzia uzito wa jeraha lake. Kwa kweli, tuna wasiwasi na tunatumai sio mbaya sana. Itabidi tusalie katika hali sawa kama awali tu katika mechi ijayo dhidi ya Cape Verde.

Baada ya mechi mbili, Misri ni ya pili kwa alama moja kwenye kundi linaloongozwa na Cape Verde kwa alama tatu. Msumbiji ni ya tatu kwa alama moja, Ghana inavuta mkia kwa alama moja.

Ghana haijashinda mechi yoyote kwenye mashindano ya  Kombe la Mataifa ya Afrika tangu mwaka 2019 nchini Misri.

Ghana itakutana na Msumbiji siku ya Jumatatu wiki ijayo katika uwanja wa Olympic d'Ebimpe jijini Abidjan. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.