Pata taarifa kuu

AFCON: Morocco yaibwaga Tanzania kirahisi (3-0)

Morocco imeshinda wazi mabao 3 kwa 0 dhidi ya Tanzania, ambayo ilimaliza ikiwa na wachezaji kumi, wakati wa mechi ya kwanza ya Kundi F ya Kombe la Mataifa ya Afrika, siku ya Jumatano huko San-Pédro nchini Côte d'Ivoire.

Nahodha Simba wa Atlas, Romain Saïss ameifungia Morocco bao la kwanza katika kipindi cha kwanza.
Nahodha Simba wa Atlas, Romain Saïss ameifungia Morocco bao la kwanza katika kipindi cha kwanza. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Bao la kwanza la Morocco limepachikwa wafuni na beki wake wa kati na nahodha Romain Saiss katika dakika ya 30, na la pili lilefungwa na kiungo wa Marseille Azzedine Ounahi katika dakika ya 77 na bao la tatu limefungwa na mshambuliaji wa Sevilla FC Youssef En- Nesyri katika dakika ya 80 za mchezo.

Tanzania, taifa la 121 la Shirikisho la Soka la Duniani (FIFA) na nchi iliyoorodheshwa katika kundi linaloundwa na timu ngumu, haikuonyesha lolote katika mchezo huu isipokuwa safu ya ulinzi  ambayo ilionekana kushindwa kulinda lango lao na kucheza vibaya, hali iliyomfanya Novatus Miroshi kuenguliwa kwa kadi mbili za njano katika dakika ya 70. Mechi ya pili ya Kundi F, ya mwisho ya siku ya kwanza, imezikutanisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo dhidi ya Zambia jioni .

Watazamaji katika uwanja wa Laurent-Pokou katika mji wa pwani wa San-Pédro walikuwa wachache kwa mechi hii iliyochezwa kwenye joto la nyuzi 30. 

Siku ya Jumapili, Morocco itakutana na DR Congo na Zambia kupepetana na Tanzania.

Morocco, iliyofungwa na Ufaransa katika nusu fainali ya Kombe la Dunia (2-0) Desemba 2022 nchini Qatar, ina AFCON moja pekee kwenye rekodi yake, mwaka 1976 nchini Ethiopia, pamoja na fainali iliyopoteza mwaka 2004 dhidi ya Tunisia, nchi mwenyeji (2-1). Wakati wa toleo la mwisho mnamo 2022 iliondolewa katika robo fainali na Misri (2-1).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.