Pata taarifa kuu

AFCON 2024: Vincent Aboubakar kutoshiriki kwenye mechi ya kwanza ya Cameroon

Akiwa amejeruhiwa katika paja la kushoto, nahodha wa Cameroon, Vincent Aboubakar, hatocheza mechi ya kwanza ya timu yake, Simba wa Nyika katika Kombe la Mataifa ya Afrika, Jumatatu dhidi ya Guinea, kulingana na uongozi wa timu hiyo ya taifa ya Cameroon.

Mchezaji wa Cameroon Vincent Aboubakar, wakati wa mechi dhidi ya Comoro, Januari 24, huko Yaoundé, ambapo Simba wa Nyika alipata ushindi.
Mchezaji wa Cameroon Vincent Aboubakar, wakati wa mechi dhidi ya Comoro, Januari 24, huko Yaoundé, ambapo Simba wa Nyika alipata ushindi. © Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji huyo wa kati mwenye umri wa miaka 31, aliye chini ya mkataba na klabu ya Uturuki ya Besiktas, alijeruhiwa katika mazoezi siku ya Ijumaa.

"Vipimo vya MRI (imaging resonance imaging) vimefanyika siku ya (Jumamosi) Januari 13, 2024 katika hospitali ya Katoliki ya St-Joseph Moscati huko Yamoussoukro na kuonyesha utengano mdogo wa musculo-aponeurotic ulioainishwa kiwango cha kwanza", ametangaza daktari wa timu ya taifa ya Cameroon katika taarifa.

"Jeraha hili dogo halisababishi kukosekana jambo ambalo linaweza kutatiza ushiriki wa mchezaji kwenye mashindano," ameongeza.

Jeraha alilopata Aboubakar lilisababisha hofu ya kupoteza kwa muda wote wa mashindano. "Hatocheza kwa mechi ya kwanza," mmoja wa maafisa kweye uongozi wa timu ya taifa ya Cameroon ameliambia shirika la habari la AFP.

Vincent Aboubakar, nahodha wa Simba wa Nyika, mshindi wa fainali ya AFCON 2017 nchini Gabon iliyotwaliwa dhidi ya Misri (2-1), amekosa muda wa kucheza tangu Besiktas ilipomuweka kando na timu hiyo, Desemba 11.

Cameroon iko katika Kundi C la toleo la 34 la AFCON, pamoja na Senegal, bingwa mtetezi, Guinea na Gambia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.