Pata taarifa kuu

AFCON 2024: Côte d'Ivoire iko tayari kuanza 'AFCON kubwa zaidi katika historia'

Kwa mara ya pili katika historia ya michuano hiyo, Ivory Coast inajiandaa kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika. Nchi imefanya uwekezaji mkubwa ili kuweza kupokea michuao hiyo na kuifanya "AFCON kuwa kubwa zaidi katika historia yake".

Mashabiki wa timu ya taifa ya Côte d'Ivoire wakiwa kwenye soko kuu la Adjamé mjini Abidjan mnamo Januari 9, 2024.
Mashabiki wa timu ya taifa ya Côte d'Ivoire wakiwa kwenye soko kuu la Adjamé mjini Abidjan mnamo Januari 9, 2024. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwanahabari wetu maalum mjini Abidjan,

Michuano hii ilikuwa ifanyike mwaka wa 2023 na hatimaye, kama toleo la awali nchini Cameroon ambalo lilikuwa limeahirishwa kwa mwaka mmoja kutokana na janga la UVIKO-19, Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Côte d'Ivoire litaanza na miezi michache ya kuchelewa kwa tarehe zilizopangwa awali Januari 13, 2024.

Kwa sababu ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar ambalo lilichezwa kwa mara ya kwanza majira ya baridi, AFCON hii nchini Côte d'Ivoire ilipaswa kufanyika mwezi Juni na Julai 2023 na si kama kawaida mwanzoni mwa mwaka. Tatizo pekee ni kwamba nchini Côte d'Ivoire ni msimu wa mvua. Tishio ambalo lilisukuma Shirikisho la Soka la Afrika kuahirisha michuano hii hadi mwezi Januari 2024. "Hatutaki kuchukua hatari ya kuwa na mashindano chini ya mafuriko. Hii haitakuwa nzuri kwa soka la Afrika na taswira yake,” Mkuu wa CAF Patrice Motsepe alijitetea.

Karibu dola bilioni na nusu ya uwekezaji

Licha ya kuahirishwa huku, Côte d'Ivoire imejipanga sawa hadi michuano hii itakapomalizika, ikiwa ni kwa amara ya pili Côte d'Ivoire kuandaa michuano hii baada ya ile ya mwaka 1984. Kukarabati miundombinu ya hoteli, barabara; vituo vya hospitali, ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo... Takriban dola bilioni moja na nusu za uwekezaji zilitumiwa ili kufanya toleo hili la 2024 kuwa "michuano mkubwa zaidi katika historia" kwa maneno ya François Amichia, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya michuano ya AFCON ( COCAN).

Msisitizo maalum umewekwa kwenye viwanja sita ambavyo vitaandaa mashindano.Uwanja wa Olimpiki wa Alassane Ouattara huko Ébimpé ambao ni mpya na una nafasi 57,000 utaandaa mechi ya ufunguzi na fainali na utatumika kama onyesho jipya kwa soka la Côte d'Ivoire. Viwanja vya Charles Konan-Banny huko Yamoussoukro, Amadou Gon-Koulibaly huko Korhogo na Laurent Pokou huko San Pedro, vyote vikiwa na uwezo wa wa kupokea watu 20,000, pia vilijengwa hasa kwa hafla hiyo. Mjini Abidjan na Bouaké, viwanja vya Félix Houphouët-Boigny na Stade de la Paix vilikarabatiwa ili kuandaa michuano hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.