Pata taarifa kuu

Kombe la Dunia 2022: Morocco yakata rufaa kwa usimamizi wa mechi yake dhidi ya Ufaransa

Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF) limetangaza Alhamisi, Desemba 15, kwamba limewasilisha malalamiko yake kwa 'chombo chenye uwezo' (bila kutaja jina) kupinga usimamizi wa mechi ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2022, ambapo Simba wa Atlas walifungwa na Ufaransa 2-0 siku ya Jumatano.

Mwamuzi Cesar Arturo Ramos akitoa onyo kwa Sofiane Boufal wakati wa mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia kati ya Ufaransa na Morocco 2022, Desemba 14, 2022.
Mwamuzi Cesar Arturo Ramos akitoa onyo kwa Sofiane Boufal wakati wa mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia kati ya Ufaransa na Morocco 2022, Desemba 14, 2022. REUTERS - HANNAH MCKAY
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, FRMF inarejea kwenye maamuzi mawili ya ussimamizi wa mechi "baada ya kuinyima Morocco penalti mbili zisizopingika kwa maoni ya wataalamu kadhaa".

Shirikisho la soka la Morocco linazungumzia kitendo kilichotokea katika dakika ya 27 wakati Sofiane Boufal na Théo Hernandez walipokutana katika eneo hilo, na ambapo mwamuzi kutoka Mexico, César Arturo Ramos, alitoa onyo kwa Morocco.

Shirikisho hilo pia limekosoa kutopigwa kwa penalti ambayo mwamuzi alikubali mwenyewe, kabla ya mapumziko, wakati Youssef En-Nesyri alijikuta amedondoshwa baada ya kugongana na Aurélien Tchouaméni. FRMF inashangaa kwamba mwamuzi kupitia video "haikujibu hali hizi". Rufaa yake kwa hakika haina nafasi ya kushinda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.