Pata taarifa kuu

Kombe la Dunia 2022: Morocco yatinga nusu fainali baada ya kuibwaga Ureno

Baada ya Uhispania katika mzunguko wa 16, timu ya Morocco imepata ushindi mkubwa tena kwa kuitoa Ureno ya Cristiano Ronaldo (1-0). Vijana wa Walid Regragui sasa wanaweka historia kwa kuwa nchi ya kwanza barani Afrika na katika ulimwengu wa Kiarabu kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia.

Yahya Attiat-Allah akikumvatiana na Youssef En-Nesyri.
Yahya Attiat-Allah akikumvatiana na Youssef En-Nesyri. REUTERS - CARL RECINE
Matangazo ya kibiashara

Uwanja wa Al Thumama mjini Doha kwa mara nyingine tena umejaa shauku kwa timu ya taifa ya Morocco, Atlas Lions. Wakati huu, vijana wa Walid Regragui wametinga nusu-fainali, ndoto isiyofikirika kwa mashabiki na wapenzi wa soka barani Afrika muda si mrefu uliopita. Baada ya kutoka hatua ya makundi wakiwa mbele na kuwaondoa Uhispania katika mzunguko wa nane kupitia mikwaju ya penalti, lolote liliwezekana kwa Simba ya Atlas. Hata hivyo Ureno ilipewa tangu hapo awali nafasi ya kushinda mchezo huo.

Youssef En-Nesiry apatishia ushindi Morocco

Dakika ya 42, Youssef En-Nesiry alitumia vyema krosi ya Yahya Attiat-Allah kwenye eneo la hatari na mshambuliaji huyo wa Morocco akafunga bao kwa kichwa huku Diogo Costa akikosa kabisa kujitambua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.