Pata taarifa kuu

Morocco yapata ushindi wa kihistoria dhidi ya Uhispania na kutinga robo fainali

Morocco imepata ushindi mkubwa kwa kuwaondoa Uhispania baada ya kutaka sare ya kutofungana (0-0:) na kuingia katika hatua ya mikwaju ya penalti ambapo Morocco iliingiza mabao (3-0) Jumanne 6 Desemba na kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Kikosi cha Morocco chasheherekea ushindi wake dhidi ya uhispania , na hivo kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia.
Kikosi cha Morocco chasheherekea ushindi wake dhidi ya uhispania , na hivo kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia. REUTERS - WOLFGANG RATTAY
Matangazo ya kibiashara

Morocco ni nchi ya nne barani Afrika kufika hatua hii ya mashindano hayo, baada ya Cameroon, Senegal na Ghana.

Morocco ambayo imefuzu katika mzunguko wa 16, zaidi ya miaka 30 baada ya kufikia hatua hii kwa mara ya kwanza mnamo 1986, imefaulu katika michuano ya kiombe la dunia mwaka huu. Lakini Simba ya Atlas haikusudii kuishia hapo baada ya kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi lililojumuisha Croatia na Ubelgiji.

Morocco ni taifa la nne la Afrika kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia baada ya Cameroon (1990), Senegal (2002) na Ghana (2010).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.